watalii wazuru Kenya

Watalii wote wa ndani na wa kimataifa ambao wako katika maeneo tofauti ya Kenya na wanahitaji kurudi nyumbani kupitia Nairobi wana hadi Jumatatu .

Waziri wa Utalii Najib Balala anasema baada ya Jumatatu hawataweza kuondoka au kuingia Nairobi kwani safari za ndani zitasitishwa kufikia Jumatatu. Ndege za kitaifa hazitaathiriwa, hata hivyo wakati wa kuwasili abiria wote lazima wawasilishe vyeti  vya COVID-19.

Maelfu ya watalii wa ndani ambao walisafiri nje ya Nairobi kujivinjari  wikendi hii sasa wamekwama baada ya kufungwa kwa kaunti za  Nairobi na kaunti zingine nne.

Mohammed Hersi kutoka KTF anasema wako kwenye hali tata kwani lazima watafute njia ya kuwasaidia kurudi nyumbani kwao. Anasema pia kufungwa kunamaanisha hakuna biashara kwao wakati wa likizo ya Pasaka kwani asilimia kubwa ya watalii wa ndani  wanatoka Nairobi.

 

Marufuku ya Safari za  ndani na nje mwa Kaunti za Nairobi, Kajiado, Machakos, Kiambu na Nakuru ambazo zilitangazwa jana na Rais Uhuru Kenyatta yanaanza hii leo. Walakini, serikali imeelezea kwamba kuwa mikoa hiyo mitano imewekwa kama eneo moja la Zoni na kwa hivyo wakaazi wa kaunti hizo wanaweza kusafiri kwa hiari ndani ya kaunti tano.

Wasafiri na waendeshaji wa PSV hata hivyo wanasema muda zaidi ulipaswa kutolewa.

View Comments