In Summary
  • Kenya imerekodi visa 1,698 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 11,352katika muda wa saa 24 zilizopita
  • Katika visa hivi vipya, 1,591 ni raia wa Kenya huku 107 wakiwa raia wa kigeni, 926 ni wa kiume na 772 ni wanawake
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe

Kenya imerekodi visa 1,698 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 11,352katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 143,063 kutoka kwa sampuli 1,542,088

Katika visa hivi vipya, 1,591 ni raia wa Kenya huku 107 wakiwa raia wa kigeni, 926 ni wa kiume na 772 ni wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana siku 17  huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 100.

Kulingana na takwimu za wizara ya afya watu 456  wamepona virusi vya corona, 267 walipona wakiwa nyumbani huku 189 wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 97,650 ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba watu 16 waliaga dunia kutokana na maambukizi kufikisha 2,292 watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 1,620 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 4,247 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 235 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU)

Watu 378,363 wamepokea chanjo ya corona kufikia siku ya jumatano.

 

 

 

 

View Comments