Ruto na rapa Khaligraph

Naibu Rais William Ruto hatimaye alijitokeza na kuamua kuwasaidia wasanii wa Kenya ambao wamekuwa wakiomba serikali ifungue nchi kwa mda sasa.

Hii ilijia baada ya rapa Khaligraph Jones (Brian Robert Ouko) kumsihi Ruto aingilie kati kwa niaba ya Wakenya ambao wamelala na njaa, hawana huduma za msingi na ajira wakati wa janga hili kwani baa, mikahawa na maeneo mengine yameathiriwa sana.

Ruto alikutana na washiriki wa tasnia ya ubunifu kujadili wasiwasi wao, kupokea maoni na mapendekezo juu ya hali yao ya sasa.

Janga la Covid-19 na changamoto zake za kiafya na kiuchumi ambazo zimeathiri nchi, na kuathiri vibaya mamilioni ya maisha, haswa katika tasnia ya hoteli ubunifu na burudani, ilitawala mashauriano hayo.

"Wasanii waliibua maswala ya wasiwasi mkubwa yanayowaathiri, walitoa ahadi ya kushiriki katika kusaidia kupunguza usambazaji wa Corona na wakatoa maoni juu ya njia bora zaidi ambayo itasaidia serikali na tasnia kupata mapato," Ruto alisema.

Miongoni mwa ombi lililotolewa ni pamoja na kuundwa kwa fedha maalum za kusaidia wasanii, serikali na watu wa nia njema ya kuiboresha tasnia hiyo katika nafasi ya dijitali kuwezesha tamasha za muziki mtandaoni na kusaidia tasnia hiyo kuzoea hali mpya ya kawaida.

Ruto akiwa katika mkutano na wasanii wa Kenya

"Tunatambua kuwa wasanii wameshirikiana na serikali na tunathamini pendekezo lao kusaidia katika kukabiliana na janga hilo," Ruto alisema.

Aliongeza kuwa alijitolea kuhakikisha kuwa mapendekezo yao yatafikishwa katika Kamati la Kitaifa la dharura la kukabiliana na janga la Corona.

Mtangazaji Jalang'o, mcheshi DJ Shiti, DJ Joe Mfalme, DJ Pierra Makena, Kristoff, Willy Paul na Nonini walikuwa miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo.

View Comments