In Summary
  • Inspekta Jenerali wa Polisi Hillary Mutyambai amesema kwamba askari wa DCI yuko mikononi mwa polisi baada ya kumshambulia askari wa trafiki
  • Mutyambai alisema kwamba afisa huyo wa DCI atashtakiwa kwa makosa ya kuendesha gari akiwa amelewa na kumshambulia afisa wa polisi
IG Hillary Mutyambai Inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutyambai
Image: MAKTABA

 Inspekta Jenerali wa Polisi Hillary Mutyambai amesema kwamba askari wa DCI yuko mikononi mwa polisi baada ya kumshambulia askari wa trafiki hii ni baada ya video ambayo imeenea sana kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha afisa wa polisi wa trafiki akisukumwa na gari hilo.

Kwenye video hiyo, askari huyo wa trafiki anaonekana akibishana na dereva ambaye alikuwa raia lakini aliendelea kuendesha gari licha ya kumuona askari huyo amesimama mbele ya gari akijaribu kumzuia.

Siku ya Jumapili, Mutyambai alisema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa raia katika video hiyo ni afisa aliyehusishwa na Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai.

 

Mutyambai alisema kwamba afisa huyo wa DCI atashtakiwa kwa makosa ya kuendesha gari akiwa amelewa na kumshambulia afisa wa polisi.

Mutyambai aliongeza kuwa michakato pia iko kwa hatua zaidi za kiutawala.

"Niliona video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ya raia anayeshambulia Afisa wa Polisi wa Trafiki. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa raia katika video hiyo ni afisa aliyehusishwa na Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai." Mutyambai alisema.

 

 

View Comments