In Summary
  • Mfanyabiashara wa Nairobi ambaye anadaiwa kupata hati miliki kwa njia ya uongo alishtakiwa Ijumaa mbele ya korti ya Milimani
  • Abdirashid Abdul Sharifow maarufu Zainulabidin Sharif alifika mbele ya Hakimu Mkuu Francis Andayi na kukana mashtaka hayo
  • Abdul aliachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu Sh100,000. Kesi hiyo itatajwa Mei 20
Abdirashid Abdul
Image: Carolyne Kubwa

Mfanyabiashara wa Nairobi ambaye anadaiwa kupata hati miliki kwa njia ya uongo alishtakiwa Ijumaa mbele ya korti ya Milimani.

Abdirashid Abdul Sharifow maarufu Zainulabidin Sharif alifika mbele ya Hakimu Mkuu Francis Andayi na kukana mashtaka hayo.

Mfanyabiashara huyo anasemekana alinunua usajili wa hati miliki kwa kukusudia kwa kujifanya kuwa ni ya kweli na ndiye mmiliki halali.

Alidaiwa kutenda kosa hilo kati ya Januari 7, 2018 na Juni 29, 2020 katika Ardhi House jijini Nairobi.

Alikabiliwa na na kosa la pili ambapo anatuhumiwa kuwa Mei 5 mwaka huu katika Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai jijini Nairobi, kwa nia ya kudanganya, alijionesha kwa Inspekta Mkuu Wanga Masake kama Zainulabidin Sharif na mmiliki aliyesajiliwa wa ardhi yenye mabishano. .

Abdul anadaiwa kutenda kosa hilo, pamoja na wengine katika makao makuu ya Wizara ya Ardhi.

Mwendesha mashtaka hakupinga dhamana yake lakini alitaka ombi kwa alama za vidole kuruhusiwa.

"Afisa wa upelelezi ananiambia mfano wa uandishi wa mkono haukuchukuliwa kutoka kwa mshtakiwa na tunahitaji pia alama za vidole vyake," wakili wa mashtaka Angela Fuchaka alisema.

Aliongeza kuwa wakati wa kukamatwa kwake na katika kituo cha polisi, mshtakiwa hakuwa katika hali nzuri ya kiafya ili kuchapishwa na saini hizo.

"Ni kweli alikaa usiku katika kituo cha polisi lakini wakili wake alimshauri asichukue alama wala kutia saini," alisema.

Kupitia wakili wake Abdul, alikuwa ameomba kusitishwa kwa kesi kwa madai kwamba amepata maagizo kutoka kwa mahakama ya Mazingira na Ardhi kwenye kesi hiyo hiyo.

Wakili wake pia alikuwa amepinga karatasi ya mashtaka akisema kuwa ilikuwa na kasoro, kwa kuwa mtu anayetajwa kwenye karatasi ya mashtaka kama almaarufu ni mtu anayejulikana na kitambulisho.

Tunahisi mashtaka yanatumia korti kuendeleza uhalifu kukusanya ushahidi kupitia mlango wa nje kwa kuuliza mfano wa saini.

“Mashtaka yana nia mbaya na mfano wa saini ni kinyume cha sheria. Shtaka mahakamani halihitaji saini za sampuli, ”korti iliambiwa.

Korti hata hivyo, iliamua kwamba shauri mbele ya Mahakama Kuu halihusiani na kesi ya jinai kwa kuwa mwendesha mashtaka alikuwa hajapewa amri.

Andayi pia aliamua kwamba polisi wana haki ya kuchukua alama za vidole kwani ni mchakato wa kisheria.

“Upande wa mashtaka unaweza kurekebisha mashtaka na sioni sababu ya kukataa upande wa mashtaka maombi hayo

Ninaamuru mtuhumiwa ajipeleke kwa DCI achukuliwe alama za vidole na sampuli za saini, ”Andayi aliamua.

Abdul aliachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu Sh100,000. Kesi hiyo itatajwa Mei 20.

 

 

 

 

View Comments