Katibu Mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna amedai kwamba kulikuwa na njama iliyopangwa vizuri ya wizi wa uchaguzi mdogo wa Jumanne huko Bonchari kwa niaba ya mgombea wa Jubilee.
Akiongea katika kituo cha kuhesabu kura cha Jimbo la Bonchari leo,Sifuna alisema alikuwa na habari kwamba masanduku manne yaliyokuwa na karatasi za kupigia kura yalikuwa yamehamishiwa kwenye makazi ya mwanasiasa mzoefu kutoka kaunti ya Kisii akisubiri kusambazwa kwa baadhi ya vituo vya kupigia kura katika Kata ya Bogiakumu ambayo anasema ina idadi kubwa zaidi ya wapiga kura waliojiandikisha.
Alionya kuwa chama hicho kiliweka utaratibu wa kuzuia majaribio yoyote ya kusafirisha karatasi hizo za kupigia kura kwenda kwenye kituo chochote cha kupigia kura.