In Summary

•"Nimetumia kipindi cha siku ya leo kuzungumza na Daktari Mukhisa Kituyi na mke wake katika makao yao. Tulilinganisha na kubadilishana mawazo kuhusiana na mambo kadhaa muhimu. Vizuri kuona familia hii" Raila aliandika

Raila Odinga na Mukhisa Kituyi
Image: Twitter

Kenya iliadhimisha siku ya maombi ya kitaifa asubuhi ya Alhamisi katika ibada iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwemo Rais Uhuru Kenyatta, Naibu rais William Ruto, Jaji Mkuu Martha Koome, maspika wa bunge za seneti na kitaifa, Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi, baadhi ya wabunge na viongozi wengine.

Hata hivyo, mtu mmoja aliyetarajiwa kuonekana katika ibada kama hiyo ya kitaifa ila akakosekana ni aliyekuwa waziri mkuu na ambaye ni kinara wa ODM, Raila Odinga. Kukosekana kwake kuliibua maswali mengi miongoni mwa Wakenya wengi wakitaka kujua ikawaje akakosekana pale.

Baadae siku hiyo, Raila alijitokeza kusema alikokuwa siku ile kupitia mtandao wa Twitter. Alitangaza kuwa alitumia kipindi cha siku ile kutembelea na kushiriki mazungumzo na aliyekuwa katibu mkuu shirika la UNCTAD, Daktari Mukhisa Kikuyi na mkewe.

"Nimetumia kipindi cha siku ya leo kuzungumza na Daktari Mukhisa Kituyi na mke wake katika makao yao. Tulilinganisha na kubadilishana mawazo kuhusiana na mambo kadhaa muhimu. Vizuri kuona familia hii" Raila aliandika kwanye akaunti yake ya Twitter mida ya saa tisa mchana.

Raila pia alichapisha picha za mkutano huo. Kituyi alijiuzulu kutoka nafasi yake ya katibu mkuu kwenye shirika la UNCTAD mwezi wa Februari mwakani na kisha kurejea nchini alipotangaza nia yake ya kuwania urais kwenye uchaguzi ujao.

Mwanasiasa huyo mwenye ana umri wa miaka 65 aliwai kuwa mbunge wa Kimilili kwa muda mrefu kutoka mwaka wa 1992 hadi 2007. Mwaka wa 2013 aliwania kiti cha useneta Bungoma ingawa akapoteza kwa Moses Wetangula kabla kujiunga na shirika la UNCTAD.

Kituyi ambaye alishangaza wengi kwa kujiuzulu na kutangaza nia yake amefanya ziara kadhaa za kujitambulisha ingawa kabla ya uchaguzi huo kufika.

View Comments