In Summary

•"Kutokana na maamuzi tofauti ya korti, rais Kenyatta hana uwezo wa kupitia, kuangalia upya au kukataa kuteua majaji ambao wamependekezwa na tume ya JSC. Uteuzi wa majaji unafaa kufanyika punde baada ya majina ya waliopendekezwa kupatiwa rais. Hatua hiyo haifai kuchukua zaidi ya siku 14" muungano wa Linda Katiba ulisema.

Muungano wa linda katiba
Image: Twitter

Muungano wa Linda Katiba umekashifu kitendo cha Rais Uhuru Kenyatta kuchagua majina ya majaji huku akitupilia mbali mengine.

Kupitia ujumbe uliotolewa siku ya Alhamisi baada ya rais kuteua majaji 34 na kutupilia mbali 6 kutoka kwa orodha ya majaji 40 aliyopewa, muungano wa Linda Katiba umesema kitendo hicho ni cha kikatili.

"Katiba hairuhusu rais kufanya chochote kingine baada ya kupokea majina yaliyopendekezwa na JSC ila kuwateua. Rais ana jukumu ndogo tu kwenye uteuzi wa majaji na ameruhusiwa tu kupitisha wote waliopendekezwa na JSC" Ujumbe wa Linda Katiba ulisoma.

Baadgi ya wanachama wa muunganoi huo ni pamoja na aiyekuwa mbunge wa Gichugu Martha Karua, mwanaharakati Boniface Mwangi, mwanauchumi David Ndii na mwanamuziki Rueben Kigame.

Siku ya Alhamisi, Rais Kenyatta alikataa kuteua Aggrey Muchelule, George Odunga, Weldon Korir na Joel Mwaura Ngugi kwenye mahakama kuu. Wawili wengine, Evans Kiago ambaye amekuwa akihudumu kama hakimu na Elizabeth Omange ambaye amekuwa akihudumu kama msajili katika mahakama kuu.

Muungano huo unaodai kulinda katiba ya 2010 pia umeashiria masikitiko kutokana na kimya cha jaji mkuu Martha Koome wakati uaminifu, uadilifu na sifa za idara ya mahakama zinatiliwa shaka na kupuuzwa na rais.

Linda Katiba imesema kuwa uteuzi wa majaji haufai kuchukua zaidi ya siku 14 baada ya JSC kumpatia rais majina ya waliopendekezwa.

ujumbe wa linda katiba
Image: hisani

"Kutokana na maamuzi tofauti ya korti, rais Kenyatta hana uwezo wa kupitia, kuangalia upya au kukataa kuteua majaji ambao wamependekezwa na tume ya JSC. Uteuzi wa majaji unafaa kufanyika punde baada ya majina ya waliopendekezwa kupatiwa rais. Hatua hiyo haifai kuchukua zaidi ya siku 14" muungano huo ulisema.

Uteuzi huu unakuja baada ya miaka mbili tangu majina ya majaji 41 kupitishwa kwa rais mwakani 2019. Mmoja kati ya 41 hao, Harrison Ogweno Okeche, aliaga mwezi wa Oktoba mwaka uliopita.

Muungano wa Linda Katiba umetangaza kucheleshwa huko kukosa maana, kukosa busara na kinyume na katiba.

"Rais anafaa kuteua majaji waliopendekwa bila ya kuchelewesha. Kukosa kwake kufanya hivyo kumekiuka vipengele kadhaa vya katiba. Jambo hili ni la kisaliti na la kufanya rais kung'atuliwa mamlakani" walidai wanaLinda Katiba.

View Comments