Mwenyekiti wa ODM wa Webuye Magharibi, Ali Waziri ameaga dunia Kifo cha Waziri kilitangazwa Jumatatu na chama cha Orange kupitia Twitter.
"Tunaomboleza kifo cha Mwanachama wetu wa Maisha na Mwenyekiti wa Tawi la Webuye Magharibi Mheshimiwa Ali Waziri,tutampeza," ODM ilisema.
Chama kilimtaja Waziri kama kiongozi anayeaminika katika mkoa wa Magharibi kwa sababu ya kujitolea kwake na kujitolea kwa ukuaji wa ODM.
Chama hicho, hata hivyo, hakijataja sababu ya kifo chake.
Ali Waziri alikuwa mwanachama mwanzilishi wa chama cha ODM.