Rais Uhuru Kenyatta amewasili Addis Ababa kwa ziara rasmi ya kikazi.
Rais alitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole Jumanne alasiri ambapo alipokelewa na maafisa wakuu wa serikali, pamoja na Waziri Mkuu Abiy Ahmed.
Uhuru, alikuwa ameandamana na Makatibu wa Baraza la Mawaziri Raychelle Omamo (Mambo ya nje) na Joe Mucheru (ICT).
Wakati wa ziara yake, Uhuru atakutana na maafisa wa serikali ya Ethiopia kujadili maswala yanayohusu pande zote.