In Summary
  • Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Kitaifa wa Walimu nchini Kenya Wilson Sossion amekanusha madai kwamba alijiuzulu  baada ya kushawishiwa na kiongozi wa ODM Raila Odinga
Katibu Mkuu wa Muungano wa KNUT Wilson Sossion

Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Kitaifa wa Walimu nchini Kenya Wilson Sossion amekanusha madai kwamba alijiuzulu kutoka kwa umoja huo baada ya kushawishiwa na kiongozi wa ODM Raila Odinga.

Akizungumza Jumatatu jioni, Sossion alisema kwamba bosi wa chama cha Orange anaheshimu demokrasia, akisisitiza kwamba alijiuzulu kutoka Knut kwa mapenzi yake mwenyewe.

"Hio ni porojo. Raila hawezi na anaheshimu demokrasia ya watu, kwa hivyo hiyo ni fitina… Ilikuwa hiari yangu mwenyewe," Sossion alisema akiwa kwenye runinga moja humu nchini.

Mbunge mteulliwa alibaini kuwa Raila ni kiongozi wa chama chake na wakati wowote wanapokuwa na mazungumzo; kawaida ni kuhusu siasa na mambo ya wafanyikazi wa Kenya bungeni.

"Nimeshinikiza nyongeza ya mishahara kwa walimu, nimeshinikiza kuajiriwa kwa walimu na nikaona kuwa nimetimiza mengi katika umoja lakini ulikuwa wakati wa mimi kuondoka," aliongeza.

Hii ni mara ya kwanza kwa bosi wa zamani wa Knut kuzungumza baada ya kutangaza kujiuzulu kutoka kwa chama cha walimu.

Sossion alijiuzulu mnamo Juni 25, baada ya miaka mitatu ya mzozo wa uongozi katika umoja na Tume ya Huduma ya Walimu.

 

 

View Comments