In Summary

•Sita hao wameomba kupewa dhamana kupitia kwa mawakili wao Danstan Omari, Omayio Aranga. Shadrack Wambui na Paul Macharia.

•Wamesema kuwa ni haki yake ya kikatiba kuachiliwa kwa dhamana kwa kuwa hakuna sababu za kulazimisha aendelee kuzuiliwa.

Polisi sita ambao walishtakiwa kwa mauaji ya ndugu wawili Embu wakiwa mahakamani
Image: MAKTABA

Polisi 6 ambao walishtakiwa kwa kosa la mauaji ya ndugu wawili kutoka Embu wametoa ombi kwa mahakama waachiliwe kwa dhamana.

Sita hao wameomba kupewa dhamana kupitia kwa mawakili wao Danstan Omari, Omayio Aranga. Shadrack Wambui na Paul Macharia.

Maafisa hao; Benson Mputhia, Consolata Kariuki, Nicholas Cheruyoit, Martin Wanyama, Lilian Chemuna na James Mwaniki wote wamekanusha mashtaka dhidi yao. Wameomba kesi hiyo kuendelezwa wakiwa nje.

Kupitia wakili Danstan Omari, koplo Mputhia amesema kuwa ni haki yake ya kikatiba kuachiliwa kwa dhamana kwa kuwa hakuna sababu za kulazimisha aendelee kuzuiliwa.

Omari alisema kuwa mteja wake ako tayari kuhudhuria kesi mahakamani bila kukosa akidai kuwa kuzuiliwa kwa mshukiwa bila sababu tosha ni ukiukaji wa katiba.

Washukiwa wamesema kuwa mashahidi, wapelelezi na wahasiriwa hawajatoa ushahidi wa kuonyesha kuwa kuna uwezekano wao kuharibu ushahidi.

Maafisa hao kwa sasa wanazuiliwa kizuizini cha Industrial Area na katika jela ya wanawake ya Lang'ata wakisubiri kesi ya dhamana kusikizwa mnamo Septemba 22.

View Comments