In Summary
  • Wakenya wanaweza kuwa wamesahau kisa hicho na kuendelea na maisha yao  lakini uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi
  • Ni takriban miezi miwili tangu ndugu 2 wa Kianjokoma kaunti ya Kiambu kudaiwa kuuawa na polisi masaa ya kafyu
Mandugu wawili wanaodaiwa kufariki mikononi mwa maafisa wa polisi
Image: HISANI

Wakenya wanaweza kuwa wamesahau kisa hicho na kuendelea na maisha yao, lakini uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi.

Ni takriban miezi miwili tangu ndugu 2 wa Kianjokoma kaunti ya Kiambu kudaiwa kuuawa na polisi masaa ya kafyu.

Emanuel na Benson walikuwa wakitoka kazini  kuelekea nyumbani walipokutana na mauti yao.

Mama yao Catherine Wawira, akiwa kwenye mahojiano na TV47, alisema kwamba tangu wanawe waage dunia hajakuwa na nguvu ya kukutana na watu.

"Tangu watoto wangu waage dunia sijawahi wala kusikia kuenda sokoni wala kuhudhuria vyama, lakini tunaachia Mungu

Benson alikuwa anapenda mambo ya upishi, naye ndugu yake alikuwa anapenda ukulima, alikuwa na kuku ambao nilikuwa nawalinda, ni ndugu ambao walikuwa na furaha sana," Alizungumza Catherine.

Kulingana na Catherine walikuwa wamepangana na mume wake wazae watoto wanne, huku akisema hata akiamua kuzaa hawezi kujifungua wanawe ambao waliaga dunia.

"Ata ukiamua kujifungua siwezi jifungua Benson ama Emanuel, huwa napita kwenye vyumba vyao vya kulala kila asubuhi na kutandika vitanda vyao hivi ndivyo huwa nakutana na wanangu ata kama hawayuko."

Catherine anatarajia kupata haki kwa wanawe.

The video could not be loaded.

Thank you for watching this video. Kindly subscribe for more content from 'Home of The Untold Stories.' *About TV47* 'TV47. is available on DStv (Channel 268), SIGNET, Gotv, BAMBA and STARTIMES. We have a diverse menu of programming. Switch on today for the best in infotainment. Give us feedback on our news, features and interviews. Also, tell us what you'd like us to bring to you. __ For Breaking News, kindly subscribe by sending NEWS to 24047. __ Connect with us: Website: https://www.tv47.co.ke/ Facebook: https://www.facebook.com/TV47KE Twitter: https://twitter.com/tv47ke Instagram: https://www.instagram.com/tv47ke/ __

 

 

 

 

View Comments