In Summary

•Mahakama ilisikia kwamba Ouko, akiwa na ufahamu halisi kwamba ana virusi vya UKIMWI alifanya ngono bila kinga na mtoto huyo kimakusudi  kinyume na sheria.

•Mshukiwa aliachiliwa kwa thamana ya Sh 500,000 huku hakimu akiamuru kesi itajwe tena  mnamo Novemba 30 na isikizwe tarehe 21 Desemba mwaka huu.

Mahakama ya Milimani mjini Nairobi

Mwanamume mmoja  mwenye umri wa makamo alifikishwa katika mahakama ya Kisumu na kukabiliwa na mashtaka matatu  ambayo ni pamoja na kutenda kitendo kiichofaa, kusambaza virusi vya UKIMWI kimakusudi na kumteka nyara kijana.

Richard Ouko alishtakiwa kwa kufanya kitendo kisichofaa cha kushika sehemu za siri za mvulana mwenye umri wa miaka 13 kimakusudi, akijua na kinyume cha sheria  kati ya tarehe 29 na 31 Oktoba 2021 katika eneo la Manyatta ndani ya Kaunti ya Kisumu.

Mahakama ilisikia kwamba Ouko, akiwa na ufahamu halisi kwamba ana virusi vya UKIMWI alifanya ngono bila kinga na mtoto huyo kimakusudi  kinyume na kifungu cha 26 (1) cha Sheria ya Makosa ya Kujamiiana.

Ouko akiwa Kondele tarehe 29 Oktoba, alimteka nyara mvulana huyo kwa nia ya kuchukua pesa kwa njia haramu kutoka kwa mamake.

Alipokuwa anashtakiwa mbele ya Hakimu Chrispine Noel Chokaa siku ya Jumatano, mshtakiwa alikanusha mashtaka yote yaliyoandikwa dhidi yake.

Mshukiwa aliachiliwa kwa thamana ya Sh 500,000 huku hakimu akiamuru kesi itajwe tena  mnamo Novemba 30 na isikizwe tarehe 21 Desemba mwaka huu.

(Utafsiri: Samuel Maina)

View Comments