In Summary

•Inasemekana wanaume hao walijaribu kumdanganya msichana huyo lakini alipokataa wakamkamata, wakumfunga na kumtupa kwenye gari kisha kuondoka kwa kasi.

• Mama wa msichana huyo ambaye alizidiwa sana na maumivu aliyopitia binti yake hakuweza kuongea.

•Alisema tayari mtu mmoja amekamatwa akiwa na gari linalodaiwa kutumiwa na wahalifu hao ambalo kwa sasa linazuiliwa.

Msichana mwenye umri wa miaka kumi na tatu kutoka Garissa ambaye alinajisiwa na genge la wanaume watano akizungumza na wanahabari. Mshukiwa mmoja amekamatwa huku familia ikitoa wito wa kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa washukiwa wengine
Image: ERICK KYALO

Familia ya msichana wa miaka 13 kutoka Garissa inatafuta haki kufuatia kunajisiwa kwa binti yao na genge la wanaume watano Ijumaa jioni alipokuwa akirejea nyumbani kutoka dukani.

Inasemekana wanaume hao walijaribu kumdanganya msichana huyo lakini alipokataa wakamkamata, wakumfunga na kumtupa kwenye gari kisha kuondoka kwa kasi.

 Alipokuwa anazungumza na wanahabari katika kituo cha polisi cha Garissa siku ya  Jumamosi, mwanafunzi huyo wa darasa la sita ambaye alioneka mwenye kuchoka, kushtuka na kuogopa alisimulia masaibu yake mikononi mwa wanajisi.

"Nilikuwa tu nimenunua maziwa saa kumi na mbili na dakika 20 jioni kutoka kwa duka ambalo si mbali sana na nyumbani kwetu wakati gari lilipopunguza mwendo lilikuja karibu nami," alisema.

 "Waliokuwemo walishusha vioo. Mmoja wao aliendelea kunisalimia nami nikaitikia."

Anasema baada ya sekunde kadhaa, wanaume wanne walitoka kwenye gari moja, wakamkamata na kumuingiza ndani.

“Niliacha hata viatu vyangu, walinipeleka porini na kuniamuru nivue nguo, nilipojaribu kupinga walinitishia kuniua,” alisema.

 Mama wa msichana huyo ambaye alizidiwa sana na maumivu aliyopitia binti yake hakuweza kuongea.

 Wanafamilia hao walielezea hasira zao wakisema kuwa wahusika lazima wafikishwe mahakamani na waadhibiwe kisheria.

MCA wa Galmagala Yusuf Omar alisema amesikitishwa na kukasirishwa na watu wanaonajisi watoto katika jamii.

“Mimi ni mtu na mzazi mwenye hasira sana ninaposimama hapa leo. Siwezi kufikiria wanaume watano wakifanya kitendo cha kinyama kama hiki kwa msichana mdogo kama huyu," Omar alisema.

"Siyo tu kwamba ni jambo la aibu lakini halifikiriki. Watu hawa lazima wakamatwe na kufikishwa mahakamani." aliongeza

 Alisema matukio ya aina hiyo yanaongezeka katika mji huo na kuwataka polisi kuongeza kasi na kuimarisha doria.

Afisa mkuu alithibitisha kuwa kisa hicho kiliripotiwa katika kituo hicho na ripoti ya matibabu kutoka kwa daktari ilithibitisha madai hayo.

Alisema tayari mtu mmoja amekamatwa akiwa na gari linalodaiwa kutumiwa na wahalifu hao ambalo kwa sasa linazuiliwa.

(Utafsiri: Samuel Maina)

View Comments