In Summary
  • TikTok inapendwa zaidi na watumiaji mtandaoni kuliko Google ambayo imeshikilia nafasi hiyo kwa miaka 10 mtawalia
  • App hiyo ina shirikisha video fupi, zinazoangazia vichekesho, densi na siasa
TikTok yaipiku Google kwa wingi wa watumiaji wa mitandao
Image: Hisani

TikTok inapendwa zaidi na watumiaji mtandaoni kuliko Google ambayo imeshikilia nafasi hiyo kwa miaka 10 mtawalia.

Mtandao huo wa kushirikisha video unatembelewa zaidi kuliko Injini ya utaftaji ya Marekani, kulingana na Cloudflare, kampuni ya usalama IT.

Viwango hivyo vinaonyesha kuwa TikTok iliiondoa Google katika nafasi ya kwanza mnamo Februari, Machi na Juni mwaka huu, na imeshikilia nafasi ya kwanza tangu Agosti.

Mwaka jana Google ilikuwa ya kwanza, na tovuti kadhaa ikijumuisha TikTok, Amazon, Apple, Facebook, Microsoft na Netflix zote zilikuwa kwenye 10 bora.

Cloudfare ilisema inafuatilia data kwa kutumia zana yake Cloudflare Radar ambayo inafuatilia trafiki ya wavuti.

Inaaminika kuwa moja ya sababu za kuongezeka kwa umaarufu wa Tiktok ni kwa sababu ya janga la Corona, kwani marufuku ya kutotoka nje ilimaanisha watu walikuwa wamekwama nyumbani na wanatafuta burudani.

Kufukia Julai mwaka huu, App ya TikTok ilikuwa imepakuliwa zaidi ya mara bilioni tatu ,kulingana na kampuni ya data ya Sensor Tower.

Mtandao huo wa kijamii unaomilikiwa na kampuni ya China inayoitwa Bytedance, sasa ina zaidi ya watumiaji bilioni moja wanaofanya kazi kote duniani, na idadi hiyo inaendelea kukua.

Nchini China, ili kuzingatia sheria za udhibiti wa nchi, programu inaitwa Douyin, na inaendeshwa kwenye mtandao tofauti.

Douyin ilizinduli awali Septemba 2016. Mwaka huu, China iliamua kwamba watumiaji walio na umri wa chini ya miaka 14 wangeruhusiwa kutumiaukuwaa hilo kwa dakika 40 kwa siku.

Hofu ya usalama

TikTok ilizinduliwa kimataifa mwaka wa 2018, baada ya kuunganishwa na huduma nyingine ya mitandao ya kijamii ya China, Musical.ly, programu ambayo iliwaruhusu watumiaji kushirikisha video zao za kusawazisha midomo (lip-synching) kwa nyimbo.

Mtando huo wa kijamii sio umekumbwa na utata mara kadhaa. Mnamo mwaka wa 2019, ilipigwa marufuku kwa muda nchini India, uchunguzi wa kijasusi wa Marekani ulibaini kuwa Musical.ly inaruhusu maudhui yaliyochapishwa na watumiaji wa umri wa chini na kutozwa faini ya pauni milioni 4.3 .

Kama moja ya App ya China iliyopata ufanisi mkubwa, wanasiasa na wadhibiti nje ya nchi hiyo wameibua wasiwasi kuhusu usalama na faragha.

Mwaka jana TikTok ililazimika kupinga madai kwamba inadhibitiwa na serikali ya China.

Theo Bertram, mkuu wa sera ya umma wa TikTok Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika, alisema itakataa ombi lolote kutoka kwa China la kukabidhi data.

App hiyo ina shirikisha video fupi, zinazoangazia vichekesho, densi na siasa.

 

 

 

 

View Comments