In Summary
  • Watu 4 wameaga dunia kutokana na maambukizi ya corona huku idadi hiyo ikifika 5,562
  • Kuna wagonjwa 711 ambao wamelazwa hospitalini, 5,563 wamejitenga nyumbani
  • Vile vile kuna wagonjwa 37 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU)
Image: HISANI

Visa 185 vya maambukizi ya corona vimerekodiwa nchini kutoka kwa sampuli 5,515 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 157 ni wakenya huku 28 wakiwa raia wa kigeni,97 ni wanaume huku 88 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 320,584 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 3.4%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,195,460.

Vile vile watu 440 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 292,357, 331 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 109 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Watu 4 wameaga dunia kutokana na maambukizi ya corona huku idadi hiyo ikifika 5,562.

Kuna wagonjwa 711 ambao wamelazwa hospitalini, 5,563 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 37 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 11,,625,788.

 

 

 

 

View Comments