In Summary

•Wafanyabiashara wanaouza kuku na mayai wanatozwa shilingi 70 za Kenya sawa na shilingi 2500 za Uganda.

Image: BBC

Wafanyabiashara wanaouza kuku na mayai wanatozwa shilingi 70 za Kenya sawa na shilingi 2500, kupata idhini ya kuingiza mayai yao nchini Kenya, jambo linalokwenda kinyume na makubaliano ya awal, limeripoti gazeti la Daily Monitor nchini Uganda.

Wafanyabiashara wengi pamoja na vyama vya wafanyabiashara wameliambia gazeti hilo kuwa tozo hilo ni miongoni mwa masharti ambayo yamewekwa dhidi ya mayai kutoka Uganda.

Haya yanajiri miezi sita baada ya Kenya kuondoa marufuku iliyokuwa imeiweka dhidi ya kuku na bidhaa za kuku kutoka Uganda kwa ajili ili kuwalinda wakulima wake na athari za Covid-19.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa mwezi Januari na Waziri wa kilimo wa Kenya Peter Munya, Waziri wa biashara Betty Maina, na Waziri wa kilimo wa Uganda Frank Tumwebaze ilionyesha kuwa Kenya itaruhusu mauzo ya mayai, kuku na vifaranga, baada ya kuzuiwa kuingia nchini Kenya tangu Februari 2021

View Comments