In Summary

•Waziri wa Kilimo Peter Munya ametetea  uamuzi wa kutoa  ushuru wa Sh2 kutoka kwa bei ya mahindi akisema ni bora kuliko bei ilivyokuwa.

•Akizungumza katika  mkutano wa wakuu wa nchi za IGAD mjini Nairobi, Munya alidokeza kuwa kuna hatua zingine zitakapochukuliwa  ilikuwaepusha Wakenya dhidi ya uhaba huo.

Waziri wa Kilimo Peter Munya
Image: HISANI

Waziri wa Kilimo Peter Munya ametetea  uamuzi wa kutoa  ushuru wa Sh2 kutoka kwa bei ya mahindi akisema ni bora kuliko bei ya awali.

Akizungumza katika  mkutano wa wakuu wa nchi za IGAD mjini Nairobi, Munya alidokeza kuwa kuna hatua zingine zitakapochukuliwa  ilikuwaepusha Wakenya dhidi ya uhaba huo.

Alisema kuwa Kenya inatazamia kushirikisha jumuiya za kikanda kama COMESA na nchi kama Zambia kusaidia katika kuongeza usambazaji wa mahindi nchini Kenya.

Kulingana na Munya,Afrika nzima pia inakabiliwa na ukame wa mzunguko na mkutano wa IGAD utakuja na masuluhisho kwa wakuu wa kanda kufanya kazi pamoja na kuja na rasilimali ili kukabiliana na suala hilo.

Alisema tayari kuna mpango ambao unatazamiwa kushirikishwa  katika sekta ya mifugo ambayo itachangia uchumi wa mkoa huo.

Akiongezea pia ni  kuwa wanatazamia kuweka hatua ambazo zitatekelezwa watakapofanya kazi pamoja kama kanda.

Haya yanajiri  baada ya  Waziri huyo kusema kwamba mfumuko wa bei ya unga wa ugali ni kutokana na tozo kama hizo ambazo serikali inatoza kwa nafaka inayoagizwa kutoka nje, jambo ambalo limefanya nafaka kuwa ghali kwa mkenya wa kawaida.

Akionekana kutoa ushauri kwa serikali, Waziri Munya alisema kwamba ni wakati sasa serikali ya Kenya ifungue njia za mawasiliano za moja kwa moja na mataifa ambako nafaka huagizwa kama vile Tanzania na majirani wake Zambia na Malawi ambako nafaka imekuwa ikiagizwa kutoka huko na wasaga nafaka nchini.

View Comments