In Summary

• Wanjigi ameikosoa serikali kufuatia mvutano wa hivi majuzi na familia ya Kenyatta kuhusu ushuru.

•Jimi alitahadharisha serikali kuwa wanaguza waya wa umeme na kuwataka wamkome Mama Ngina.

Jimi Wanjigi akizungumza baada ya kujiunga na chama cha Safina 9/Machi/2022
Image: Ezekiel Aming'a

Aliyekuwa mgombea urais kupitia chama cha Safina, Jimi Wanjigi, ameikosoa serikali kufuatia mvutano wa hivi majuzi na familia ya Kenyatta kuhusu ushuru.

Suala la kukwepa ushuru limeibua hisia mseto miongoni mwa wanananchi huku baadhi ya viongozi wakihusisha familia ya hayati Jomo Kenyatta. Raila Odinga Jimi Wanjigi na Seneta wa Narok Ledama Ole Kina ni baadhi ya  viongozi ambao wameikosoa serikali kwa hatua ambazo wamechukua dhidi ya familia ya Kenyatta na Moi.

"Hii shida hamtatatua mkitafuta mali ya Jomo Kenyatta‚na hayupo. Hilo hatuta ruhusu. Kama mnashida na Uhuru  Kenyatta‚Uhuru ni Uhuru ‚mtafuteni yeye lakini babake hapana, " alisema Jimi siku ya Jumapili.

Wanjigi aliongezea kwa kubainisha kuwa Jomo Kenyatta  hayupo na hawezi kujitetea. "Bibilia pia  inasema tuwalinde wajane na yatima. Mama Ngina ni mjane kwa nini mnamtafuta. Kijana angali yupo mtafute yeye. Muachane na hiyo ya historia. Ya Jomo Kenyatta na mama hatutaki kuskia‚

Jimi alitahadharisha serikali kuwa wanaguza waya wa umeme na kuwataka wamkome Mama Ngina. " Kama mnajarbu kuchukua mali ya Jomo Kenyatta ata  mbele yetu sisi. Sisi ni kina nani? Kesho yaweza kuwa wewe kesho kutwa mimi ama mwingine.''

Jimi alizungumza hayo siku ya Jumapili alipotangamana na washirika wa Furaha Worship Centre ‚Kiambu kuabudu nao.

Siku ya Jumamosi, Februari 4‚ Mama Ngina alivunja kimya baada ya madai ya familia yake kukwepa ushuru mwanawe Uhuru Kenyatta alipokuwa rais.  

"Hakuna haja ya kuharibia wengine majina na mimi ndio watu wasikike wanafanya kazi. Hapana, Mtu ashtakiwe, alipe kile anatakiwa kulipa," Mama Ngina alisema.

Aliongezea kwa kuidhubutu serikali kupiga mnada mali yake iwapo atapatikana na kosa la kutotekeleza wajibu wake wa kulipa ushuru.

"Na Kama ni mimi, hata kama sijalipa kwa mwaka mmoja, mali ichukuliwe ilipe ushuru kwa sababu ni lazima. Hakuna haja ya kufanya kazi ya kisiasa ya hapa na kule. Na Si kweli kwamba sijalipa ushuru. Na watu wanajua hawasemi ukweli," aliongeza.

Rais William Ruto akizungumza Jumapili katika Kanisa la Deliverance Church International mjini Ruai, Nairobi alisema kuwa Wakenya wote wamekubaliana kila mtu alipe ushuru.

Sote tumekubaliana kwamba hakutakuwa na watu wakubwa, sote ni sawa mbele ya sheria na Katiba na wote tutalipa kodi kulingana na mapato yetu. Hilo ni jambo la kupongezwa kwa sababu hatutaangalia kabila, tabaka, dini au wewe ni kijana au mzee tunapojadili masuala ya ushuru,” alisema.

View Comments