In Summary

•Allister Brown, mwenye umri wa miaka 45, alivuka rekodi yake ya awali ya kupiga ngoma kwa saa 134 na dakika tano, kwa kupiga ngoma kwa zaidi ya saa 150.

•"Siku zote nilikuwa na jambo hili akilini mwangu nilitaka kufanya hivi katika kumbukumbu ya Sharon."

Image: BBC

Mwanaume mmoja wa Lisburn amevunja rekodi ya dunia kwa kupiga ngoma kwa muda mrefu.

Allister Brown, mwenye umri wa miaka 45, alivuka rekodi yake ya awali ya kupiga ngoma kwa saa 134 na dakika tano, kwa kupiga ngoma kwa zaidi ya saa 150.

Alimaliza "mbio hizo za kupiga ngoma," siku ya Jumamosi alasiri, baada ya kuanza Jumapili iliyopita, zaidi ya wiki moja.

Bw Brown aliamua kufanya hivyo kama sehemu pia ya kumkumbuka rafiki yake, marehemu Sharon Deegan, ambaye aliaga dunia kutokana na saratani ya kongosho Januari 2021, akiwa na umri wa miaka 49.

Akiongea Jumamosi alasiri, katika Kituo cha Muziki cha Lisburn ambapo aliweka rekodi zake zote tatu za dunia, Bw Brown alisema kuwa imekuwa "kazi kubwa".

Alisema kuwa kumbukumbu za Bi Deegan, pamoja na uungwaji mkono wa marafiki zake, zilimfanya aendelee vyema zoezi hilo.

"Asante kwa kila mtu ambaye ameniunga mkono," alisema.

"Siku zote nilikuwa na jambo hili akilini mwangu nilitaka kufanya hivi katika kumbukumbu ya Sharon."

Bw Brown amewahi kuvunja rekodi ya dunia mara mbili ya muda za kupiga ngoma kwa muda mrefu, kwanza mwaka wa 2003 alipopiga ngoma kwa saa 58, kabala ya kuibunja mwaka wa 2008 alipodumu kwa saa 103 tu na sasa ya tatu kapiga ngoma kwa saa 150.

Sheria za Rekodi za Dunia za Guinness zinasema kwamba kwa kila saa ya kupiga ngoma Bw Brown anaruhusiwa kupumzika kwa dakika tano.

Hakupumzika dakika zake tano kwa saa kadhaa na kumruhusu kuchukua muda mrefu zaidi wa kupumzika.

Lakini kufikia Ijumaa asubuhi, siku tano baada ya jaribio lake la kuvunja rekodi, rafiki wa Bw Brown, na mratibu wa tukio hilo, Duncan Campbell, alisema mpiga ngoma huyo alikuwa amelala kwa takriban saa mbili tu wakati wa zoezi hilo la kuweka rekodi mpya ya dunia.

View Comments