In Summary
  • Alisisitiza kuwa hakuna Mkenya anayefaa kutengwa na serikali licha ya matokeo ya kura.
  •  
  • Rais William Ruto ameelezea uamuzi wake wa kumuunga mkono aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga kwa wadhifa wa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika kwa .
RAIS WILLIAM RUTO
Image: TWITTER

Rais William Ruto amekariri msimamo wake kumuunga mkono aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga kwa wadhifa wa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika kwa mara ya kwanza tangu wawili hao wakutane nchini Uganda Jumatatu, Februari 26.

Akiongea wakati wa Kongamano la Uwekezaji katika Kaunti ya Homa Bay mnamo Jumanne, Februari 27, Ruto aliwakumbusha wakaazi kwamba kila mara amekuwa akitayarisha mpango wa kuunganisha taifa baada ya uchaguzi wa urais wa 2027 uliokumbwa na utata.

Alisisitiza kuwa hakuna Mkenya anayefaa kutengwa na serikali licha ya matokeo ya kura.

Mkataba huo uliafikiwa nchini Uganda huku wawili hao wakiwa wenyeji wa Rais Yoweri Museveni.

"Nilikuwa hapa Homa Bay wakati wa kampeni na niliwaahidi kuwa hakuna atakayeshindwa hapa Kenya, niliahidi kwamba nitajitahidi sana kuhakikisha kila mtu anapata nafasi, hamkuniamini, sasa mnaona. Mambo yanaendaje.Si niliahidi hilo sokoni?

"Kuna nafasi kwa ajili yetu sote. Hushindi kwa kuwafanya wengine washindwe. Tunataka hali ya ushindi kwa Wakenya wote. Hakuna Wakenya walio katika upinzani na walio serikalini,"  rais alieleza.

Hii ilikuwa mara ya kwanza  Ruto kutoa maoni yake kuhusu azma ya Raila kuwania uwenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika (AUC). Raila, mnamo  siku ya Jumatatu, aliwasifu Ruto na Museveni kwa kuunga mkono ombi lake, na wakati huo huo akamtambua hasimu wake kisiasa kama Rais wa Kenya.

"La muhimu zaidi, kwa kuhimizwa na Rais Museveni, tulijadili pia juu ya kugombea kwangu uwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika. Ninamshukuru sana Rais Museveni kwa kuniuga mkono na kwa Rais Ruto kwa kuniunga mkono kikamilifu," Raila alieleza.

View Comments