In Summary
  • "Hongera sana Jacque Maribe. Mungu akubariki unapomtumikia Asante Moses Kuria kwa kusimama na kizazi, naomba uendelee kutenda mema na kunyoosha mkono wako," Itumbi alisema.
Jaque Maribe
Image: Instagram

Aliyekuwa mtangazaji wa televisheni, Bi Jacque Maribe ameteuliwa kuwa mkuu wa mawasiliano katika wizara ya Utumishi wa Umma, utendaji na usimamizi wa utoaji huduma.

Uteuzi huu umeonekana kuibua hisia mseto miongoni mwa Wakenya, baadhi wakionekana kushangaa, wengine wakimfurahia kwa kupata kazi hiyo huku wengine hata wakikosoa uteuzi huo.

Miongoni mwa watu walioonekana kufurahia hatua ya Maribe kupata kazi hiyo ni rafiki yake Dennis Itumbi.

Itumbi alizamia kwenye mitandao ya kijamii kumpongeza rafiki yake. Alipongeza kitendo cha CS Kuria cha kumpa mwanahabari huyo wa zamani nafasi ya kuendelea na kazi yake.

"Hongera sana Jacque Maribe. Mungu akubariki unapomtumikia Asante Moses Kuria kwa kusimama na kizazi, naomba uendelee kutenda mema na kunyoosha mkono wako," alisema.

Tazama maoni mengine kutoka kwa baadhi ya Wakenya kuhusu uteuzi mpya wa Maribe;

Steve Mulwah wa Kite. Baba John: So fast,  ama wacha ninyamanze it's Monday....

Justice Mathenge: Mungu nifundishe kunyamaza

Brian wattanga: @LydiahKinyanju4 kumbe alishatengewa kazi kitambo.

Kiraguemilio@gmail@Kiraguemiliogm1 :Yes, she is a Kenyan like everybody else. The court declared her innocent.

Husgang@Mahusde28: Juana na watu...hii mambo good conduct ni ya watu hawana pesa.

Boniface Muko@MukoBoniface: Every person deserves a second chance.

Mutembei William@Mutembeiwiliam: Congratulations maribe.

uez,ENG@Muez_ENG: So does she have a good conduct certificate?!

Eric@_Chucky72: Waah kumbe the game is always rigged.

014.@ROGUEKENYAN: at this point, NOTHING they do surprise me anymore, I've lowered my expectations to below 0

Haya yanajiri mwezi mmoja baada ya kuachiliwa kwa kosa la mauaji na haki Grace Nzioka aliyempata Bw. Irungu na hatia.

Jowie atahukumiwa Machi 13 baada ya hukumu kuahirishwa wiki iliyopita.

View Comments