In Summary

•Jeff aliuawa na simulizi za yeye kuwa na mawazo ya kujitoa uhai ni za kupotosha, babake Peter Ngugi aliambia wachunguzi.

•"Kwake (DJ Fatxo), hatua hiyo ilikuwa muhimu sana ili kusiwe na mashahidi," Ngugi alisema.

Babake Jeff Mwathi Peter Ngugi, mamake Anne Mwathi na wakili wao Danstan Omari katika chumba cha mahakama ya Milimani mnamo Juni 8, 2023.
Image: DOUGLAS OKIDDY

Mbunifu wa mapambo ya ndani Jeff Mwathi aliuawa na simulizi za yeye kuwa na mawazo ya kujitoa uhai ni za kupotosha, babake Peter Ngugi aliambia wachunguzi.

Jeff, ambaye jina lake halisi ni Geoffrey Mwathi Ngugi alifariki mnamo Februari 22, 2023, katika ghorofa ya Redwood mtaa wa Roysambu, Nairobi.

Inadaiwa kuwa alianguka hadi kufa katika hatua ya kujitoa mhanga. Hiyo ilikuwa baada ya usiku wa kunywa pombe na mwanamuziki DJ Fatxo, jina halisi Lawrence Njuguna Wagura.

Wawili hao walikuwa wamekutana Februari 21 kwa kazi ya usanifu wa mambo ya ndani katika biashara ya DJ Fatxo kando ya barabara ya Eastern Bypass.

Baadaye waliburudika kwa vyakula na vinywaji katika baa na vilabu mbalimbali kabla ya kuenda kupumzika katika nyumba ya Fatxo mwendo wa saa tisa usiku wa kuamkia Februari 22.

Nyumba hiyo ilikuwa kwenye orofa ya 10 ya ghorofa ya Redwood ndani ya Roysambu.

Babake Jeff alipokuwa akitoa ushahidi mbele ya hakimu wa Milimani, Rose Ndomi wakati wa kusikizwa kwa uchunguzi Jumatano alisema mwanawe alikuwa na DJ Fatxo kwenye baa. Walikuwa na wanawake watatu.

Ngugi alisema DJ Fatxo kisha akamwita dereva wake Geoffrey Wanyeki aje kwenye baa ili amrudishe nyumbani akidai alikuwa amelewa sana kuwa kwenye usukani.

"Wanyeki hakuja peke yake. Alikuja na binamu ya Njuguna (DJ Fatxo) Christopher Wang'ombe. Kisha waliendelea kunywa licha ya kusema alikuwa amelewa sana," Ngugi alithibitisha.

Wakati walipokuwa wakitoka kwenye baa hiyo kuelekea nyumbani, Wanyeki hakuendesha gari.

Badala yake, alikuwa DJ Fatxo ambaye aliendesha gari lake nyumbani na Jeff na wanawake watatu.

Wanyeki na Wang'ombe walitumia njia nyingine kufika kwenye nyumba hiyo.

Babake Jeff Ngugi alihoji kwa nini walikuwa wakienda kwa DJ Fatxo ilhali kazi ya kuendesha gari ambayo Wanyeki aliitiwa haikuwa muhimu tena.

Akiwa ndani ya nyumba, DJ Fatxo alimwomba Jeff ajiudhuru na kujilaza kitandani kwake kwa sababu alionekana kusinzia kupita kiasi.

"Wao (DJ Fatxo, Wanyeki na Wang'ombe) walimfuata hadi chumbani. Kulikuwa na zogo kidogo pale na ni wakati huo ambapo Jeff aliuawa," Ngugi aliambia uchunguzi.

Alieleza kuwa DJ huyo aliporudi kutoka chumbani, aliwataka wanawake hao waondoke haraka na akajitolea kuwarudisha nyumbani.

"Kwake (DJ Fatxo), hatua hiyo ilikuwa muhimu sana ili kusiwe na mashahidi," Ngugi alisema.

Baada ya DJ Fatxo kurudi, hakwenda nyumbani.

Akabaki ndani ya gari katika eneo la maegesho. Wakati fulani, Wanyeki na Wang'ombe walionekana wakitoka nyumbani na Wanyeki kwenye simu.

Walizungumza kwa dakika kadhaa wakiwa nje ya jengo lakini ndani ya kiwanja kabla ya kurejea nyumbani.

Ngugi aliambia wachunguzi kuwa ilikuwa yapata saa kumi na moja na dakika arobaini asubuhi wakati wawili hao walionekana kwenye lifti wakielekea kwenye nyumba hiyo.

"Kisha saa 5.47 asubuhi, mwili wa Jeff unanaswa katika picha za CCTV ukidondoka kutoka nyumbani. Ni watu hawa wawili walioulazimisha mwili wa Jeff kupitia dirishani," Ngugi alisema.

Alisema dirisha lilikuwa dogo sana kwa Jeff kujipenyeza na kwamba ni baadhi ya watu wangeweza kumtoa nje kwa nguvu.

"Hata jinsi alivyoanguka inaonyesha tayari alikuwa amekufa kwa sababu mwili uligonga ardhini na kuruka kisha ukalala tambarare, kumaanisha kuwa tayari ulikuwa hauna uhai," Ngugi aliongeza.

Alimtaka hakimu awatafute hao watatu; DJ Fatxo, Wanyeki na Wang'ombe wana kesi ya kujibu kuhusiana na mauaji ya Jeff.

Hapo awali ilidaiwa kwamba Jeff alitoweka chumbani na baadaye mwili wake usio na uhai ukapatikana kwenye ghorofa ya chini ya nyumba hiyo.

Hata hivyo, ushahidi wa babake Jeff unalingana na matokeo ya awali ya DCI ambayo yaliondoa uwezekano wa marehemu kujilazimisha kupitia dirishani.

Wapelelezi pia walikuwa wamegundua kuwa kulikuwa na mzozo ndani ya nyumba hiyo baada ya uchunguzi wa kisayansi.

Jeff, 23, alizikwa mnamo Machi 3, 2023, katika eneo la Likia, Njoro, kaunti ya Nakuru.

Mwili wake hata hivyo ulitolewa kwa uchunguzi wa pili baada ya mamlaka kuamuru uchunguzi wa mauaji dhidi ya kifo hicho.

Kesi ya uchunguzi itaendelea tarehe 1, Oktoba.

Baadhi ya mashahidi 35 wanatarajiwa kutoa ushahidi wao. Kufikia sasa, ni watatu tu wametoa ushuhuda wao.

Hao ni wazazi wa Jeff Peter Ngugi na Ann Mwathi na mjomba aliyefariki Muchoki Mwathi.

View Comments