In Summary

• Rais Uhuru aongeza muda wa kafyu kwa siku 60

Rais Uhuru Kenyatta
Image: PSCU

Muda wa kafyu nchini Kenya umeongezwa tena kwa siku 60 zaidi.

Rais Uhuru Kenyatta  siku ya Jumanne, Juni 29, alitangaza kuongeza muda wa kafyu  kote nchini.

Akizungumza kutoka ikulu Nairobi, Uhuru alitangza kuwa kaunti 13 ambazo zimetangazwa kuwa maeneo hatari ya maambukizi ya Covid-19 zitaendelea na kafyu ya kuanzia saa moja usiku hadi saa kumi asubuhi kwa siku sitini zijazo.

Kaunti hizo  13 Homa Bay, Migori, Kisumu, Siaya, Busia, Kakamega, Vihiga, Bungoma, Kisii, Nyamira, Kericho, Bomet na Trans Nzoia.

 

Muda wa kafyu katika maeneo mengine utasalia kama hapo awali kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi asubuhi.

Maelekezo ya mazishi ni ndani ya saa 96 huku hafla za harusi zikiruhusiwa watu 100 pekee.

 

 

(Mhariri: Davis Ojiambo).

View Comments