In Summary
  • Wanafunzi Kadha walazwa Hospitalini baada ya  Bweni kuteketea kwa Moto katika shule ya wasichana ya Buruburu
Bweni la shule la upili ya wasichana ya buruburu yateketea
Image: Hisani

Bweni laKingdom katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Buruburu limeteketea kwa moto.

Kulingana na wanafunzi hao, moto huo ulianza wakati wa burudani mwendo wa saa 4:30 jioni.

Baadhi ya wanafunzi walikuwa ndani wamelala huku wengine wakiwa ndani ya boma hilo.

Idadi ya wasichana wamekimbizwa katika Hospitali ya Metropolitan ambayo ni jirani na shule hiyo.

Kulingana na mwanafunzi wa kidato cha nne, moto uliwashwa kwenye kila ghorofa ya bweni la Kingdom  ambalo ni jengo la orofa tatu.

Baadhi ya wanafunzi waliokuwa ndani, waliruka kutoka bwenini moto ulipoanza.

Polisi pia wamewazuia wazazi kuingia kwenye boma hilo.

Kulingana na mwalimu mkuu, Caroline Maina, alisema moto ulikuwa katika humba kimoja kati ya vyumba 45 na moto huo ulidhibitiwa.

Alieleza zaidi kuwa alikuwa na kikao na kidato cha kwanza na cha pili na baadaye alikula chakula cha mchana kabla ya kuarifiwa kuhusu tukio hilo.

"Nilikuwa na baraza la kidato cha kwanza na cha pili kuanzia asubuhi hadi saa 2:30 usiku ambapo nilikuwa nimewaalika washauri ili kuzungumza na wanafunzi. Nilichelewa kula chakula cha mchana saa 3-4 na washauri na kuwatembeza hadi getini," alisema.

Aliongeza, "Nilipokuwa nikirudi nyuma, mwalimu alinijia akiniarifu kuwa bweni moja lilikuwa linawaka moto."

Maina alisema kuwa wasichana hao waliingiwa na hofu na wale waliojeruhiwa wamepelekwa hospitalini.

"Sina orodha kamili ya walio hospitalini lakini shule ikishafika, tutawapa taarifa wazazi," alisema.

Mkuu wa shule amewataka wazazi kuwaacha watoto wabaki shuleni. Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.

Mengi yafuata;

 

 

View Comments