In Summary

• Ruto aliambia mkutano huo kuwa kuna haja ya dharura kushughulikia suala la malimbikizi ya malipo ambayo takriban asilimia 60 ni malipo ya uzeeni. 

• Mdhibiti wa Bajeti alifichua kuwa uzalishaji wa mapato katika kiwango cha kaunti ni hatua ambayo inaweza kufungua uwezo wa kiuchumi wa serikali za kaunti.

Naibu rais William Ruto akiongoza mkutano wa IBEC, Jumanne.
Image: twitter.com/WilliamsRuto

Hazina ya kitaifa imetoa zaidi ya Shilingi bilioni 286 za mgao wa serikali za kaunti mwaka huu wa kifedha. 

Katika kikao cha Baraza la Bajeti na Uchumi (IBEC) kilichoongozwa na Naibu Rais William Ruto katika Makazi yake ya Karen siku ya Jumanne, Hazina ya kitaifa ilisema kuwa shilingi biioni 85 ambazo hazijatolewa zinashughulikiwa kwa haraka ili zitumwe kwa kaunti. 

Gavana wa Turkana Josphat Nanok ambaye alihudhuria mkutano huo alisema utoaji wa pesa hizo kwa wakati utarahisisha utoaji wa huduma katika serikali za kaunti. 

Image: Twitter.com/WilliamsRuto

Waliohudhuria kikao hich walikuwa Gavana Josphat Nanok, Naibu Waziri wa Ugatuzi Julius Korir, Mdhibiti wa Bajeti Margaret Nyakang’o, wawakilishi kutoka Hazina ya Kitaifa, Wizara ya Ugatuzi na Wanachama wa Kamati Tendaji ya Kaunti. 

Ruto aliambia mkutano huo kuwa kuna haja ya dharura kushughulikia suala la malimbikizi ya malipo ambayo takriban asilimia 60 ni malipo ya uzeeni. 

"Wizara ya Ugatuzi itaitisha mkutano na washikadau ili kujadili suala hili tata kwa nia ya kulitatua na kuondoa adhabu zisizo za kila mara," alisema. 

Image: Twitter.com/WilliamsRuto

Mdhibiti wa Bajeti alifichua kuwa uzalishaji wa mapato katika kiwango cha kaunti ni hatua ambayo inaweza kufungua uwezo wa kiuchumi wa serikali za kaunti. 

"Tumeshirikiana na Hazina ya Maendeleo ya Mitaji ya Umoja wa Mataifa ili kuongeza mapato ya kaunti ambayo pia yatazisaidia kushughulikia suala la bili ambazo hazijalipwa," Dkt Nyakang'o alisema.

View Comments