logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Shahada ya Sakaja kutoka Uganda yabatilishwa

Shahada ya Sakaja imetiliwa shaka huku walalamikaji wanne wakidai kuwa ni ya kughushi.

image
na

Makala15 June 2022 - 07:50

Muhtasari


•Barua kutoka kwa tume inasema imepokea taarifa muhimu kuhusu uhalisi wa Shahada ya Kwanza ya Sayansi katika Usimamizi.

•Uhalisi wa Shahada ya Sakaja kutoka Chuo Kikuu cha Team umehojiwa huku walalamikaji wanne wakidai kuwa ni ya kughushi.

Seneta wa Nairobi na mgombea ugavana Johnson Sakaja akizungumza katika Karen wakati wa chakula cha jioni cha Iftar mnamo Aprili 21, 2022.

Tume ya Elimu ya Vyuo Vikuu (CUE) imebatilisha kutambuliwa kwa shahada ya Seneta wa Nairobi Johnson Sakaja kutoka Chuo Kikuu cha Team nchini Uganda.

Barua kutoka kwa tume iliyoandikwa tarehe Juni 14 inasema imepokea taarifa muhimu kuhusu uhalisi wa Shahada ya Kwanza ya Sayansi katika Usimamizi.

Tume hiyo inasema shahada hiyo itahitaji uchunguzi zaidi ili kubaini uhalali wa shahada hiyo.

"Kwa hivyo, kwa mujibu wa taratibu za utambuzi wa CUE, tunabatilisha kutambuliwa kwa shahada yako kutoka chuo kikuu kilichotajwa," mwenyekiti wa CUE Chacha Nyaigoti Chacha alisema.

Mnamo Juni 6 tume hiyo ilimwandikia Sakaja  barua ikithibitisha kutambuliwa kwa cheti chake kutoka Team University.

Uhalisia wa Shahada ya Sakaja kutoka Chuo Kikuu cha Team umehojiwa huku walalamikaji wanne wakidai kuwa ni ya kughushi.

Malalamishi hayo yaliibuka punde baada ya IEBC kumuidhinishwa Sakaja kuwania kiti cha ugavana wa Nairobi kwa tikiti ya UDA mnamo Juni 7.

Mmoja wa walalamishi, Dennis Wahome, anadai  kwamba Sakaja hakuwahi kusoma wala kufuzu kutoka Chuo Kikuu cha Team.

Alidai kuwa Cheti cha Shahada ya Sakaja ya Sayansi katika Usimamizi kutoka Chuo Kikuu cha Team  ilichapishwa mnamo Mei 29, 2022.

Wahome aliendelea kusema Sakaja hakuwahi kufuzu kutoka Chuo Kikuu mnamo Oktoba 21, 2016 kama alivyodai kwa vile jina lake halimo kwenye orodha ya wahitimu wa chuo hicho.

Alidai, Chuo Kikuu cha Team kilifutilia mbali kozi ya Shahada ya Sayansi katika Usimamizi mnamo 2015, mwaka mmoja kabla ya madai ya kuhitimu kwa Sakaja.

Seneta huyo, hata hivyo, ameshikilia kuwa stakabadhi zake za kitaaluma ni halali.

Kesi hiyo iko mbele ya Kamati ya Kusuluhisha Mizozo ya IEBC ambayo uamuzi wake unatarajiwa wakati wowote.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved