In Summary
  • Uamuzi huu umewasilishwa kwa Sakaja Johnson Arthur na ana haki ya kukata rufaa
Johnson Sakaja,baada ya kujiwasilisha katika makao makuu ya DCI
Image: RADIO JAMBO

Tume ya Elimu ya Vyuo Vikuu kwa mara nyingine tena imebatilisha shahada ya seneta wa Nairobi Johnson Sakaja.

Katika barua kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, CUE ilisema hadi kukamilika kwa uchunguzi wa uhalisi wa shahada hiyo iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Team nchini Uganda, mgombea ugavana hakuwa amewasilisha uthibitisho wowote.

"Kulingana na matokeo haya na kuambatana na masharti ya vifungu vya Sheria ya Vyuo Vikuu, 2012, sehemu ya XI ya Kanuni za Vyuo Vikuu 2014, Viwango na Miongozo ya Vyuo Vikuu, 2014, na Viwango vya utambuzi na usawazishaji na kutokana na tashwishi katika cheti cha utambuzi kilichotolewa, Tume imefikia uamuzi usioepukika kwamba cheti kinachodaiwa kuwa cha Shahada ya Sayansi katika Usimamizi (ya Nje ya nchi) hakistahiki kutambuliwa," barua hiyo inasema.

Uamuzi huu umewasilishwa kwa Sakaja Johnson Arthur na ana haki ya kukata rufaa.

"Tume inakutaarifu kwamba utambuzi wa kufuzu kwa Shahada ya Kwanza ya Sayansi katika Usimamizi (ya nje ya nchi)  inayodaiwa kutoka Chuo Kikuu cha Team, iliyotolewa kwa Sakaja Johnson Arthur, ambayo iliwasilishwa kwa ofisi yako kulingana na hitaji la kifungu cha 22( 2) cha Sheria ya Uchaguzi na Kanuni ya 47 ya  sheria za Uchaguzi (Mkuu) za 2012 imetupiliwa mbali," barua iliyoonekana na meza yetu ya habari inasoma.

 

 

View Comments