In Summary

•Maafisa wanasema inaweza kuchukua muda mrefu kufika orofa ya chini na kwamba hawajui ni watu wangapi bado wamenaswa humo.

•Hili ni tukio la hivi punde kutokea katika eneo hilo na tasnia ambayo inalaumiwa kwa ukosefu wa usimamizi na uchoyo wa wakandarasi.

Jengo la orofa saba linalojengwa laporomoka huko Kirigiti katika Kaunti ya Kiambu mnamo Septemba 26, 2022.
Image: Twitter

Watu wawili waliuawa na saba kuokolewa baada ya nyumba ya ghorofa sita iliyokuwa ikijengwa kuporomoka katika eneo la Kirigit, Kaunti ya Kiambu Jumatatu.

Nyumba hiyo iliangukia kwenye nyumba ya makazi chini yake ikiwanasa baadhi ya waliokuwa pale.

Polisi wanasema baadhi ya wafanyikazi walikuwa wamefika kazini wakati mjengo huo ulipoanguka.

Polisi kufikia saa 9 alfajiri walikuwa wametoa miili miwili na kuwaokoa wengine saba wakati shughuli hiyo ikiendelea.

Timu ya mashirika mengi iko katika eneo la tukio kuwaokoa waathiriwa kutoka kwa vifusi.

Maafisa wanasema huenda ikachukua muda mrefu kufika ghorofa ya chini na kwamba hawajui ni watu wangapi bado wamenaswa humo.

Hili ni tukio la hivi punde zaidi kutokea katika eneo hilo na sekta hiyo ambayo inalaumiwa kwa ukosefu wa usimamizi na uchoyo wa wanakandarasi.

Mkuu wa DCI wa Kiambu Richard Mwaura alisema wanachunguza tukio hilo. "Sasa tunalenga kuwaokoa waathiriwa na tutawashughulikia waliosalia baadaye," alisema.

Wanajeshi ni miongoni mwa mashirika katika eneo la tukio.

Gazeti la The Star limebaini kuwa gavana wa Kiambu Kimani Wamatangi alikuwa miongoni mwa wahudumu wa kwanza kwenye eneo hilo, na kuhakikisha kuwa shughuli za uokoaji zimeratibiwa vyema.

 

Zaidi ya kufuata...

View Comments