In Summary

• Ndege hiyo ilipata hitilafu muda mfupi baada ya kupaa na kulazimika kutua katika eneo la Kimana, kaunti ya Kajiado.

Mwanariadha David Rudisha
Image: Facebook

Helikopta ndugu iliyokuwa imembeba mwanariadha mashuhuri wa Kenya David Rudisha ilipata ajali katika mbuga ya wanyama ya Amboseli jioni ya Jumamosi Desemba 10.

Katika ripoti ambayo ilichapishwa na Big Life Foundation kwenye ukurasa wa Facebook, ndege hiyo ilipata hitilafu muda mfupi baada ya kupaa na ikalazimika kutua kwa kishindo katika mbuga hiyo huku watu kadhaa wakiripotiwa kuumia.

Rudisha ambaye anashikilia rekodi ya mbio za mita 800 kwa wanaume alikuwa akisafiri na watu wengine ambao ripoti hiyo haikubainisha walikuwa wangapi lakini ilisema kuwa hawakupata majeraha ya kuhatarisha afya zao.

“Muda mfupi baada ya kupaa kutoka kwenye uwanja wa ndege karibu na mahali ambapo Michezo ya Olimpiki ya Wamasai ilikuwa ikifanyika leo, ndege nyepesi iliyokuwa imembeba David Rudisha, mshikilizi wa Rekodi ya Dunia ya mita 800, na watu wengine kadhaa waliounganishwa kwenye hafla ya leo, ililazimika kutua kwa dharura,” sehemu ya ripoti hiyo ilisoma.

Mtu mmoja tu ndiye aliyejeruhiwa vibaya huku wengine akiwemo Rudisha wakipata majeraha madogo na kuwa wako katika hali nzuri.

“Mmoja wa abiria alijeruhiwa na amelazwa hospitalini kwa matibabu. Wengine, akiwemo Bw. Rudisha, ambaye ni mlezi wa Olimpiki ya Wamasai, hawakupata majeraha yoyote ya kimwili. Kama ilivyo kawaida kufuatia ajali yoyote inayohusisha ndege, Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Kenya itachunguza. Hadi wamekamilisha ripoti yao, haifai kutoa maoni zaidi,” Big Life Foundation ilisema.

 

View Comments