In Summary
  • Kujiuzulu kwake kunajiri miezi michache tu baada ya Dkt Ruto kubatilisha uteuzi wa Francis Muthaura kama mwenyekiti wa bodi ya KRA
Kamishna jenerali wa KRA, Githii Mburu
Image: Maktaba

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Ushuru ya Kenya Githii Mburu amejiuzulu.

Mwenyekiti wa Bodi Anthony Mwaura aliwasilisha uamuzi huo kwenye taarifa kwa vyombo vya habari siku ya Alhamisi akisema kuwa Mburu alikuwa amewasilisha barua yake ya kujiuzulu ili kuendeleza maslahi mengine ya kibinafsi.

"Kufuatia kujiuzulu, bodi imemteua FCCA, CS Rispah Simiyu, Wakili wa EBS, kuwa Kaimu Kamishna Mkuu KRA kuanzia tarehe 23 Februari, 2023 hadi wadhifa huo ujazwe," Mwaura alisema.

Kujiuzulu kwake kunajiri miezi michache tu baada ya Dkt Ruto kubatilisha uteuzi wa Francis Muthaura kama mwenyekiti wa bodi ya KRA.

Nafasi ya Muthaura ilikabidhiwa kwa Anthony, aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya uchaguzi ya United Democratic Alliance.

 

 

 

 

View Comments