In Summary
  • Alikuwa anatafutwa kwa madai ya uchochezi. Hii ni kuhusiana na mkutano wa wiki jana katika kiwanja cha Kamukunji jijini Nairobi
Pingu
Image: Radio Jambo

MCA wa Korogocho Absalom Odhiambo alikamatwa Jumatatu na polisi alipokuwa akisubiri kuhojiwa na maafisa wa Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC).

Polisi waliandamana naye hadi afisi za NCIC katika mtaa wa Upper Hill ambapo walimpeleka kwa ajili ya kuhojiwa.

Alikuwa anatafutwa kwa madai ya uchochezi. Hii ni kuhusiana na mkutano wa wiki jana katika uwanja wa Kamukunji jijini Nairobi.

Haijulikani kwa ni nini hasa anahitajika. Duru za habari zinasema alipelekwa katika makao makuu ya DCI kwa ajili ya kuhojiwa kabla ya kufunguliwa mashtaka.

Hatua ya polisi kufika NCIC kwa magari ya siri ilizua hisia mseto mtandaoni huku wengi wakisema ni onyesho la kurejea kwa ukatili wa polisi.

Maelfu ya watu walihudhuria mkutano huo ambapo viongozi wa Azimio walitoa hotuba kupinga dhuluma za kisiasa na haswa uchaguzi uliohitimishwa.

Walisema kuwa kura ziliibiwa.

NCIC ilimwita Odhiambo almaarufu Mobimba kwa madai ya matamshi ya uchochezi aliyotoa wakati wa mkutano wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya katika uwanja wa Kamukunji

View Comments