Polycarp Igathe ambaye kwa sasa anawania ugavana Nairobi kwa tikiti ya chama cha Jubilee ni miongoni mwa Wakenya wachache wenye bahati ya kubadilisha kutoka kazi moja hadi nyingine kwa urahisi mno.
Jamaa huyo anatajwa kuwa na bahati kwani nyadhifa nyingi ambazo ameaminiwa kuzishikilia ni za hadhi ya katika mashirika mbali mbali tajika kuendesha shughuli zao muhimu.