13 April 2023 1 Min Read
Safari ya siasa ya Bahati: Kutoka kujiunga na Jubilee, kulia kwa kupokonywa tiketi hadi kuingia UDA
Mwimbaji huyo alijiunga na chama tawala cha UDA mnamo Aprili 12, 2023.
In Summary
•Bahati aliwania kiti cha ubunge wa Mathare kwa mara ya kwanza mwaka jana ila akalambishwa sakafu.
Bahati ambaye aliwania kiti cha ubunge wa Mathare kwa tiketi ya Jubilee katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana alikaribishwa kwenye UDA siku ya Jumatano na katibu mkuu wa chama hicho Cleophas Malala.
Katika uchaguzi wa mwaka jana, Bahati aliibuka wa tatu katika kinyang’anyiro cha ubunge wa Mathare huku Anthony Oluoch wa ODM akichukua ushindi. Billian Ojiwa wa UDA alimaliza katika nafasi ya pili.
Hilo lilikuwa ni jaribio la Bahati la kwanza kuwania kiti cha kisiasa nchini Kenya.