In Summary

• Wawili hao walikuwa katika mahusiano ya kimapenzi kuanzia mwaka wa 2021 baada ya kupatana wakati wa majaribia ya kuigiza katika kipindi cha Zora.

• Jackie ana watoto wawili mmoja wao akiwa wa muigizaji mwenza Blessing.

Image: ROSA MUMANYI

Jumanne, Jackie Matubia alithibitisha mahusiano yake na muigizaji mwenza Blessing Lung’aho yametamatika baada ya muda wa zaidi ya miezi miwili ya kudokeza kuwa mambo huenda yakawa mabaya katika mahusiano yao.

Muigizaji huyo wa zamani wa kipindi cha Zora akiwaarifu wafuasi wake katika akuanti yake ya Instagram , alisema sasa anajivunia kuwa singo matha.

"Proud single mother of two," Jackie aliandika kwenye instastory yake.

Wawili hawa wamekuwa wakitoa vidokezo vya kila aina kwamba huenda mapenzi yao na baba wa mtoto wake wa pili, Blessing Lung’aho yalivunjika.

Mnamo alhamisi, Jackie alidai kuwa wanaume walimjazia maombi ya kutaka kuwa kwenye mahusano naye baad ya kutangaza kuwa singo.

View Comments