In Summary

•Mchanganuzi Mutahi Ngunyi ametangaza kwamba amehamia upande wa serikali na sasa atamuunga mkono Rais William Ruto.

•Mutahi Ngunyi sio mshawishi wa kisiasa wa kwanza kuhama kambi baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana

Washawishi wa kisiasa waliohamia Kenya Kwanza kutoka Azimio
Image: HILLARY BETT

Mchanganuzi mashuhuri wa masuala ya kisiasa Mutahi Ngunyi ametangaza kwamba amehamia upande wa serikali na sasa atamuunga mkono Rais William Ruto.

Wakati akitangaza hatua yake mpya siku ya Jumatatu, Ngunyi ambaye hapo awali alifanya kazi kama mshauri wa Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta kuhusu masuala ya kisiasa alisema hapo awali alikuwa amemhukumu Ruto vibaya.

"Taarifa kwa umma: Nimehamia kwa William Ruto. Nilimhukumu vibaya kwa kutumia jicho la nasaba. Lakini ukweli ukibadilika, lazima ubadili mawazo yako," Ngunyi alisema kwenye Twitter.

Aliongeza, "Na mpumbavu pekee ndiye habadili mawazo yake. Nilianzisha mradi wa  #HustlerNation. Sasa lazima niukamilishe. Je, kuna swali? #RutosMountainPlan.”

Hapo awali, Ngunyi alikuwa mkosoaji mkali wa utawala wa Ruto ingawa katika siku za hivi majuzi alijishusha chini na kuanza kumwomba 'kukaa ngumu' (aendelee kuwa na msimamo) hata upande wa upinzani ulipozidisha maandamano ya kupinga serikali mitaani.

Ngunyi sio mshawishi wa kisiasa wa kwanza kuhama kambi baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Grafiki ya leo inaorodhesha baadhi ya washawishi wa kisiasa waliohama katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

View Comments