In Summary

•Tasnia ya bongo ilimuomboleza mmoja wao, mwibaji Haitham Kim ambaye alifariki katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke  Ijumaa.

•Marehemu alizikwa mnamo Septemba 4 katika makaburi ya Kisutu katika hafla ya mazishi iliyojaa hisia.

Haitham Kim Mfahamu staa wa bongo aliyefariki Ijumaa.
Image: HILLARY BETT

Mwishoni mwa wiki jana, tasnia ya bongo ilimuomboleza mmoja wao, mwibaji Haitham Kim ambaye alifariki katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke siku ya Ijumaa.

Mwimbaji huyo alifariki akiwa na umri mdogo baada ya kushambuliwa na tatizo la upumuaji, hali iliyopelekea kulazwa ICU kabla ya kuaga.

Alizikwa Septemba 4 katika makaburi ya Kisutu katika hafla ya mazishi iliyojaa hisia ambayo ilihudhuriwa na wasanii wenzake, familia, marafiki na mashabiki.

View Comments