Wasanii wa Bongo wameendelea kuonyesha ubunifu mkubwa jukwaani wakati wakitumbuiza katika tamasha la Wasafi Festival 2023 linaloendelea.
Baadhi ya wasanii waliofanya ubunifu jukwaani ni pamoja na bosi wa Wasafi Diamond Platnumz, Mbosso, Zuchu, Rayvanny, Whozu na Lavalava.
Miongoni mwa mambo ya kibunifu ambayo wasanii mbalimbali wameweza kufanya ni pamoja na kutengeneza mandhari ya kijijini jukwaani, kupandishwa jukwaani kwenye jeneza na kuvaa sare za shule.