In Summary

•Miles aligusa mioyo ya wengi baada ya kuandika ujumbe wa hisia kwa Safaricom akiomba kampuni hiyo kumsaidia bintiye wakati akifariki.

•Mkewe aliwaomba watu wenye nia njema kuendelea kusaidia familia ili iweze kumzika mpendwa huyo wao kiheshima

Danny Miles
Image: HISANI

Mapema mwaka huu, Danny Miles, mwanaume aliyekuwa anapambana na saratani aligusa mioyo ya wengi baada ya kuandika ujumbe wa hisia kwa Safaricom akiomba kampuni hiyo kumsaidia bintiye wakati akifariki.

Miles, kupitia mtandao wa Facebook alifahamisha kampuni hiyo kuwa alihisi kama kwamba mwisho wake unakaribia na akaeleza wasiwasi wake kuhusu hatima ya bintiye mdogo ambaye alikuwa anakaribia kuingia shule.

Alisema kuwa ugonjwa ulitumia pesa zote alizokuwa ameweka kwa ajili ya familia na kumuacha kutegemea msaada wa marafiki.

"Habari Safaricom, mimi ni Maurice Ochieng anayejulikana kama Danny Miles. Ninatoka mjini Muhoron. Mwezi Machi mwaka jana, niligunduliwa na saratani, sarcoma ya tishu laini. Inanitafuna hakika.

Siku kwa siku ninahisi. Nilikuwa nikiweka akiba ili nipeleke familia yangu ndogo kwa likizo lakini nimeishiwa na nguvu, siwezi. Ninaishi kwa msaada wa marafiki. Binti yangu mdogo bado ni mchanga. Bado hajaanza shule. Nilikuwa nafanya mpango lakini nasikitika nimeshindwa kama baba. Mkono wangu wa kushoto ulikuwa umekatwa lakini bado saratani ilizidi kuniathiri

Ninawaomba msaidie binti yangu mara tu nitakapoondoka kwa sababu ninaweza kuhisi. Nambari yangu ni 0706345827. Namba ya mke wangu ni 0757084605 (Florence Odege) au labda mtupeleke safari ya mara moja maishani nitashukuru sana,"  Danny Miles alindikia kampuni ya Safaricom mnamo Januari 19.

Kwa bahati mbaya, Miles aliweza kukata roho siku ya Jumanne baada ya ugonjwa kukithiri.

Taarifa kutoka kwa familia ilisema aliaga dunia hospitalini mwendo wa saa nne usiku.

"Kwa wote ambao mmekuwa nami katika safari hii kuhakikisha Danny anajisikia vizuri, nawashukuru nyote. Kwa bahati mbaya hakufanikiwa, alifariki jana saa nne usiku," mkewe Miles aliandika kwenye Facebook.

Aidha, aliwaomba watu wenye nia njema kuendelea kusaidia familia ili iweze kumzika mpendwa huyo wao kiheshima.

Miles alikuwa amelazwa katika hospitali hiyo mapema mwezi huu baada ya afya yake kuzorota.

"Leo Mapema niliazwa tena katika Nyumba ya Muhoroni Rachar Nursing Home. Nilishambuliwa kwenye mapafu na sikuweza kupumua vizuri. Niko imara sasa hivi tu. Tunatafuta njia ya jinsi baadhi ya taratibu zinavyoweza kufanywa ili nipumue vizuri tena. Asante kwa Maombi na msaada wa kifedha," aliandika mnamo Machi 11.

Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wameendelea kumuomboleza kijana huyo na kuunga mkono familia hiyo changa iliyoachwa nyuma.

View Comments