In Summary

  • Baada ya kurudishwa  twitter  rais huyo  alishutumu "shambulio baya" la waandamanaji waliovamia bunge la Congress.

  •Matamshi yaTrump yameonekana kwa mara yake ya kwanza kukubali kwamba alishindwa katika uchaguzi wa mwezi Novemba.

Rais wa Marekani amesema kwamba yuko tayari kuachilia madaraka kwa amani siku moja tu baada ya wafuasi wake kushambulia bunge la Congress na kuvutia shutuma kali duniani.

Baada ya kurudishwa katika mtandao wa twitter kufuatia kufungiwa kwa saa 12, rais huyo wa chama cha Republican alishutumu "shambulio baya" la waandamanaji waliovamia bunge la Congress.

Alizungumza huku viongozi wa chama cha Democrats wakimtaka kuondolewa afisini siku 13 kabla ya muhula wake kuisha.

Katika video hiyo hakutaja kuhusu madai yake ya awali kuhusu wizi wa kura ambayo yaliwachochea wafuasi wake sugu kupiga kambi nje ya ikulu ya Whitehouse.

Wakati wa mkutano huo aliwaambia wafuasi hao kuelekea katika jumba la Capitol Hill ambapo waliingia ndani kwa lazima.

Matamshi ya rais Trump yameonekana kwa mara yake ya kwanza kukubali hadharani kwamba alishindwa katika uchaguzi wa mwezi Novemba.

Mwezi Novemba alikataa kukubali kushindwa baada ya kutuma ujumbe wa twitter kuhusu rais mteule Joe Biden kwamba alishinda kwasababu kura ziliibwa.

Trump alisema nini ?

Bwana Trump alirudi katika twitter siku ya Alhamisi jioni , kufuatia kufungiwa kwa muda kwa akaunti zake kwa saa 12, baada ya kampuni hiyi ya mtandao wa kijamii kusema kwamba jumbe zake zinachochea ghasia .

Katika kanda hiyo mpya ya video alisema: Sasa bunge la Congress limeidhinisha matokeo na sasa utawala mpya utaingia tarehe 20 Januari.

Lengo langu sasa ni kuhakikisha kuwa mchakato wa kukabidhi madaraka unafanyika kwa njia ya amani.

''Wakati huu tunahitaji maridhiano. Pia aliwapongeza wafuasi wake na kuwaahidi kwamba safari yao ndio imeng'oa nanga''.

Polisi wamekosolewa vikali kwa jinsi walivyoshughulikia ghasia hizo.

Picha zilizonaswa ndani ya bunge zilionesha vile waandamanaji walivyokuwa wanaingia katika baadhi ya sehemu za bunge bila kuzuiliwa na yeyote.

Mmoja wao alionekana akiingia katika ofisi ya Spika Pelosi na kuweka muguu yake juu ya dawati lake.

Mkuu wa polisi pia amepewa likizo ya lazima baada ya mwanamke mmoja kupigwa risasi hadi kufariki duniani katika sakafu ya bunge la wawakilishi.

Mwanamke huyo amesemekana kwamba alikuwa wanajeshi.

Shirika la Ujasusi linatafuta waliohusika na uvamizi huo na pia wizara ya sheria inasema waliokamatwa huenda wakakabiliwa na makosa manne.

Kuanzia Alhamisi, maafisa wameanza kuzungusha uzio katika maeneo ya bunge.

Ni kina nani waliofariki dunia?

Kufikia Jumatano watu wanne walikuwa wamethibitishwa kufariki dunia.

Polisi imesema pia watu watatu Benjamin Philips, 50 kutoka Pennsylvania; Kevin Greeson, 55, kutoka Alabama; na Rosanne Boyland, 34, kutoka Georgia - walifariki dunia wakendelea kupata huduma ya kwanza.

Familia ya Greeson inasema jamaa yao alifariki dunia kwa mshtuko wa moyo.

Ashli Babbitt, 35, ni sehemu ya walioingia bungeni wakati mjadala wa kuidhinisha ushindi wa Bwana Biden ukiwa unaendelea na alipigwa risasi na kufa papo hapo.

media caption'Treason, traitors and thugs' - the words lawmakers used to describe Capitol riot

Alhamisi jioni, mbunge Dean Phillips, wa Democrat huko Minnesota, aliandika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter akisema kuwa afisa mmoja wa polisi amefariki dunia.

Rais mteule wa Amerika Joe Biden

Hata hivyo, idara ya polisi baadaye ilisema kuwa taarifa hizo sio sahihi.

"Ingawa baadhi ya maafisa walijeruhiwa na kulazwa hospitali, hakuna ambaye amefariki dunia," taarifa ya polisi ilisema.

Jumatano polisi ilisema kuwa maafisa 14 wamepata majeraha.

Mmoja wao alipata majeraha mabaya ya kichwa mwingine aliangukiwa na kifaa kilichokuwa juu.

Pia afisa mwingine alihitaji matibabu ya hospitali baada ya kuburutwa hadi kwenye umati wa waandamanaji na kushambuliwa.

Walichotekeleza maafisa wa polisi?

View Comments