In Summary
  • Mkuu wa zamani wa usalama wa aliyekuwa rais wa Uganda Milton Obote, aliyedhaniwa kufa, amerejea nyumbani nchini Uganda baada ya miaka 50
  • Vincent Obodo, 81, ambaye aliwahi wakati mmoja kuongoza idara ya ulinzi katika ofisi ya rais, alikutana na wake zake wawili na watoto Ijumaa

Mkuu wa zamani wa usalama wa aliyekuwa rais wa Uganda Milton Obote, aliyedhaniwa kufa, amerejea nyumbani nchini Uganda baada ya miaka 50.

Vincent Obodo, 81, ambaye aliwahi wakati mmoja kuongoza idara ya ulinzi katika ofisi ya rais, alikutana na wake zake wawili na watoto Ijumaa

Ndugu zake hawakuwahi kumuona tangu mare ya mwisho mwezi Januari mwaka 1971-wakati serikali ya Rais Obote ilipopinduliwa, mapinduzi yaliyoongozwa na Idi Amin.

 

Familia na marafiki walilia machozi ya furaha wakati Bw. Obodo aliposindikizwa nyumbani na mfanyakaziiiii wa Shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, gazeti la Daily Monitor limeripoti.

Bw. Obodo ambaye alikuwa akiishi uhamishoni nchi jirani ya Tanzania kwa kipindi cha miongo mitano aliliambia gazetila serikali la New Vision kuwa amefurahi kurudi nyumbani.

Obote alipinduliwa na jeshi alipokuwa safarini Singapore kwa ajili ya mkutano wa jumuia ya madola.

Bw.Obodo amesema wakati huo alikuwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta akisubiri kurudi kwa Obote kutoka Singapore ndipo alipojua kuhusu kufanyika kwa mapinduzi.

Obote alikwenda uhamishoni Tanzania, na hivyo ndivyo Bw. Obodo alipojikuta Tanzania, na kusalia huko hata baada ya Bw. Obote kurejea tena madarakani mwaka 1980- ingawa alipinduliwa tena mwaka 1985.

Safari yake kurejea Uganda imeratibiwa kwa ushirikiano wa serikali ya Uganda na Tanzania, afisa wa UNHCR Carol Kibuka aliliambia gazeti.

View Comments