In Summary
  • Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amepigwa kofi usoni wakati wa ziara rasmi ya kusini mashariki mwa Ufaransa
  • Wanasiasa wamekashifu haraka tukio hilo
Image: Reuters

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amepigwa kofi usoni wakati wa ziara rasmi ya kusini mashariki mwa Ufaransa.

Kwenye video inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, Bwana Macron anaonekana akitembea kwenda kwa kizuizi katika safari ya kwenda Tain-l'Hermitage nje ya jiji la Valence.

Mwanamume anampiga kofi bwana Macron usoni kabla ya maafisa kuingilia haraka. Rais, wakati huo huo, anakimbizwa kupelekwa eneo salama.

Wanaume wawili wamekamatwa kufuatia tukio hilo, kulingana na vyombo vya habari vya Ufaransa.

Wanasiasa wamekashifu haraka tukio hilo.

Kiongozi wa mrengo wa kushoto Jean-Luc Mélenchon aliandika katika twitter "mshikamano na Rais" mara tu baada ya kiongozi huyo kushambuliwa kwa kofi .

Rais Macron kwa sasa anafanya ziara nchini Ufaransa na alikuwa ametembelea shule ya hoteli huko Tain-l'Hermitage. Ziara yake katika eneo hilo ilipangwa kuendelea Jumanne, maafisa walisema, na safari ya taasisi ya ufundi kwa vijana walio na miaka umri wa miaka 25-30.

Ziara ya rais inakuja usiku wa kuamkia hatua kubwa kwa baa na mikahawa ya Ufaransa, ambayo itaweza kufunguliwa tena kwa wateja wa ndani baada ya miezi saba ya kufungwa. Amri ya kutotoka nje wakati wa usiku nchini Ufaransa pia inasongeshwa nyuma siku ya Jumatano kutoka saa tatu hadi saa tano usiku

 

 

 

 

View Comments