In Summary

•Papa Francis amesema kuwa utoaji mimba ni "mauaji", hata muda mfupi baada ya kupata ujauzito.

Image: GETTY IMAGES

Papa Francis amesema kuwa utoaji mimba ni "mauaji", hata muda mfupi baada ya kupata ujauzito.

Hatahivyo alionekana kuwakosoa baadhi ya Maaskofu wa Kanisa katoliki wa Marekani kwa kushugulikia msimamo wa rais wa Marekani Joe Biden wa kuunga mbono utoaji mimba kwa njia ya kisiasa badala ya njia ya kitume.

Papa Francis aliyasema hayo ndani ya ndege alipokuwa safarini kutoka nchini Slovakia Jumatano.

Akizungumza kuhusu mjadala wa Maaskofu wa Marekani, kuhusu iwapo Rais Biden , ambaye ni Mkatoliki anapaswa kukataliwa kushirikik Komuniyo(Ekaristi), kwasababu anaunga mkono haki ya wanawake kuchagua kutoa mimba, hata kama yeye anapinga hilo, Papa Francis alisema:

"Sitawahi kumzuwia mtu yeyote kupokea Komuniyo, lakini sikuwahi kufahamu kwamba nina mtu mbele yangu kama kama wewe unayemuelezea, hilo ni ukweli ," alisema, bila kufafanua zaidi.

"Komuniyo sio tuzo kwa watu wasio na kasoro ya dhambi ... Komunio ni zawadi, uwepo wa Yesu na kanisa lake ," alisema Papa Francis.

"Utoaji mimba ni mauaji… Wale wanaotoa mimba wanaua ," alisema.

"Katika wiki ya tatu baada ya mwanamke kupata mimba, mara nyingi hata wakati mama hajatambua (kuwa ana unjauzito), viungo vyote vya mwili tayari huwa vimeanza kukua. Ni maisha ya binadamu.Kweli!. Na haya maisha ya binadamu yanapaswa kuheshimiwa. Ni wazi kabisa ," alisema.

"Kisayansi, ni maisha ya binadamu," alisema Papa Francis.

Mwezi Juni mwaka jana Mkutano Mkuu wa Maaskofu wa Kanisa Katoliki la Roma nchini Marekani walipigia kura taarifa ya muswada juu ya ushiriki wa Komuniyo ambao unaweza kuwazuwia wanasiasa kushiriki Komuniyo akiwemo Rais Biden

View Comments