In Summary
  • Wabunge wa upinzani nchini Uganda washitakiwa kwa ugaidi

Waendesha mashitaka wa Uganda wamewaongezea mashitaka zaidila ugaidi pamoja na pamoja na kusaidia ugaidi wabunge wawili wa chama cha upinzani- National Unity Party (NUP).

Wabunge hao - Mohammed Ssegirinya na Allan Ssewanyana, ambao ni washirika wa kiongozi wa upinzani Bobi Wine – walikuwa meshitakiwa kwa makosa matatu ya mauaji na shitaka moja la kujaribu kuua linalohusiana na mauaji yaliyotokea katika eneo la kati la Uganda la Masaka.

Walifika mbele ya hakimu mkazi wa Masaka kwa njia ya video kutoka katika gerezani katika wilaya ya Wakiso.

Wabunge hao hawakujibu lolote kuhusiana na mashitaka hayo.

Jumla ya watu 23 hadi sasa wameshitakiwa kwa mauaji ambayo watekelezaji wake wanawalenga kwa mapanga zaidi wazee wanaoendelea na kazi nyumbani au wanaofanya kazi usiku.

Kikosi cha pomoja cha maafisa wa usalama kwa sasa kinafanya uchunguzi katika eneo hilo.

Mashambulio ya aina hiyo yalitokea katika eneo hilo hilo katika miaka ya 2009, 2017 na 2018.

 

 

 

 

 

View Comments