In Summary

• Bomu hilo, lililosheheni misumari na shaba, lililenga mkahawa wa nyama ya nguruwe nje kidogo ya mji mkuu, polisi walisema Jumapili.

Polisi wa Uganda walinda eneo la mlipuko huko Komamboga, kitongoji kilichopo viungani mwa kaskazini mwa Kampala, Uganda Oktoba 24, 2021. Picha: REUTERS

Kundi la Islamic State limedai kuhusika na shambulio la bomu lililoua angalau mtu mmoja katika mji mkuu wa Uganda Kampala Jumamosi usiku, kundi hilo la wanamgambo lilisema katika taarifa iliyochapishwa katika kituo chake cha Telegram siku ya Jumapili.

Kundi hilo lilisema kwamba baadhi ya wanachama wake walilipua kilipuzi katika baa ambapo "wanachama na wapelelezi wa serikali ya Uganda walikuwa wakikutana" mjini Kampala.

Bomu hilo, lililosheheni misumari na shaba, lililenga mkahawa wa nyama ya nguruwe nje kidogo ya mji mkuu, polisi walisema Jumapili.

Habari za kijasusi zilionyesha kuwa wanaume watatu, waliojifanya wateja, walitembelea mkahawa huo, wakaweka begi la chuma chini ya meza na kuondoka muda mfupi kabla ya mlipuko huo, polisi walisema.

Mlipuko huo uliua mhudumu mwenye umri wa miaka 20 na kujeruhi watu watatu, wawili kati yao walikuwa katika hali mbaya, polisi walisema dalili zote zinaonyesha kitendo cha ugaidi.

Rais Yoweri Museveni alisema shambulio hilo "linaonekana kuwa kitendo cha kigaidi".

Mnamo mwaka wa 2010, kundi la wanamgambo wa  al Shabaab waliua makumi ya watu huko Kampala katika shambulio la bomu, wakisema ilikuwa ikiiadhibu Uganda kwa kupeleka wanajeshi nchini Somalia.

View Comments