In Summary

• Wanachama wote wa Baraza Kuu - wanaosimamia mabadiliko ya utawala wa kidemokrasia – wameondolewa kutoka kwa nyadhifa zao, alisema.

• Pia alivunja serikali zote za majimbo na kuwaondoa magavana kutoka nafasi zao.

Image: Nichola Mandil

Mkuu wa Baraza Kuu la Sudan Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan amevunja baraza hilo na baraza la mawaziri na kutangaza hali ya hatari nchini kote.

Alitoa tangazo hilo kwenye hotuba ya moja kwa moja kupitia televisheni.

Wanachama wote wa Baraza Kuu - wanaosimamia mabadiliko ya utawala wa kidemokrasia – wameondolewa kutoka kwa nyadhifa zao, alisema.

Pia alivunja serikali zote za majimbo na kuwaondoa magavana kutoka nafasi zao.

Alisema kuwa serikali ya muda itatangazwa kabla ya mwisho wa Novemba, na kutangaza kwamba uchaguzi mkuu wa kufungua njia ya serikali ya kiraia utafanyika mnamo Julai 2023

Wakati huo huo Muungano wa Ulaya umetoa wito kwa viongozi wa kijeshi na wa kiraia nchini Sudan‘’kurejesha tena’’ mchakato wa mpito nchini Sudan.

Hii inafuatia ripoti kwamba jeshi linaendelea na mchakato wa kuchukua mamlaka ya nchi.

Mkuu wa masuala ya kigeni wa EU Josep Borrell alituma ujumbe wa Twitter Jumatatu kwamba alikuwa anafuatilia matukio nchini humo kwa "hofu kubwa ".

Jeshi la Sudan halijatoa kauli yoyote kuhusu ripoti kwamba viongozi wa kiraia, akiwemo Waziri Mkuu Abdallah Hamdok, wamefungwa na wanajeshi kifungo cha nyumbani.

View Comments