In Summary

•Mhadhiri huyo wa masuala ya uchumi katika Chuo Kikuu cha Hassan I  alipatikana na hatia ya tabia chafu miongoni mwa mashtaka mengine.

Image: GETTY IMAGES

Profesa wa chuo kikuu cha Morocco anayeshutumiwa kwa kuwapa wanafunzi alama nzuri kama malipo ya upendeleo wa ngono amefungwa jela kwa miaka miwili.

Ni hukumu ya kwanza katika msururu wa kesi za unyanyasaji wa kijinsia maarufu katika vyuo vikuu nchini Morocco.

Mhadhiri huyo wa masuala ya uchumi katika Chuo Kikuu cha Hassan I, karibu na Casablanca, alipatikana na hatia ya tabia chafu miongoni mwa mashtaka mengine.

Wasomi wengine wanne watafikishwa mahakamani siku ya Alhamisi kama sehemu ya kashfa hiyo.

Kesi hizo ziliangaziwa na vyombo vya habari vya Morocco mwaka jana baada ya wanahabari kuchukua jumbe zilizoripotiwa kuwa kati ya wanafunzi na wahadhiri.

Wanaharakati wanasema ni nadra kwa kesi za unyanyasaji wa kijinsia kufikishwa mahakamani.

View Comments