Edward Lowassa
Image: BBC

Aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo anaendelea na matibabu baada ya kufanyiwa upasuaji wa tumbo.

Akizungumza jana, Ijumaa Januari 28, 2022, Mtoto wa mwanasiasa huyo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Fredrick Lowassa alisema baba yake alilazwa katika hospitali hiyo baada ya kupatwa na matatizo ya tumbo.

Taarifa kutoka kwa mwanafamilia huyo zimesema kuwa kiongozi huyo amelazwa katika hospitali hiyo kwa karibu wiki nzima baada ya kufanyiwa upasuaji.

"Baba alilazwa Muhimbili kama siku tano zilizopita. Alifanyiwa upasuaji wa tumbo, lakini bahati mbaya alipatwa na changamoto kidogo,” amesema Fredrick.

Fredrick aliwaomba watanzania kuendelea kumuombea ili afya yake iendelee kuimarika.

View Comments