In Summary

• Mkuu wa shirika la habari la CNN, Jeff Zucker, amejiuzulu kutoka shirika hilo baada ya madai kuibuka kwamba alikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mmoja wa wafanyikazi katika CNN

• Katika taarifa ya kuachia ngazi kwake, Zucker alisema kwamba anajutia kusema ukweli kwamba alikuwa katika mahusiano ya kimahaba na mfanyikazi ambaye alidinda kabisa kumtaja

Aliyekuwa rais wa CNN Jeff Zucker
Image: HISANI

Mkuu wa shirika la habari la CNN, Jeff Zucker, amejiuzulu kutoka shirika hilo baada ya madai kuibuka kwamba alikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mmoja wa wafanyikazi katika CNN.

Madai yanayomhusisha Zucker kuwa na urafiki wa kimapenzi na mmoja wa wafanyikazi katika shirika hilo yaliibuka wakati wa uchunguzi dhidi ya aliyekuwa mwanahabari katika shirika hilo Chris Cuom ambaye alifutwa kazi kwa madai ya kumsaidia nduguye  gavana wa New York, Andrew Cuom vkukwepa uchunguzi ya ukatili kwa wanawake.

Katika taarifa ya kuachia ngazi kwake, Zucker alisema kwamba anajutia kusema ukweli kwamba alikuwa katika mahusiano ya kimahaba na mfanyikazi ambaye alidinda kabisa kumtaja.

“Niliulizwa kuhusu uwezekano wa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mfanyikazi mwenza ambaye nimefanya kazi naye kwa zaidi ya miaka 20. Ninakubali ni kweli mahusiano hayo yalianza miaka ya hivi karibuni. Niliulizwa kufichua yalianza lini lakini nilidinda kufichua. Nilikosea,” Zucker alisema katika kumbukumbu iliyotumiwa wafanyikazi wote wa shirika hilo.

Habari za kujiuzulu kwa Zucker zilipokelewa kwa mshtuko mkubwa na wafanyikazi katika shirika hilo hata ingawa siku za hivi karibuni kumeonekana  kuwa mambo hayako sawa katika ngazi za juu za uongozi wa shirika la CNN.

Hata ingawa Zucker hakuwa amemtaja mwanamke huyo ambaye alidaiwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi naye, Allison Gollust ambaye ni mwanamke afisa mkuu wa masoko katika kampuni hiyo alifichua kwamba ni yeye ambaye alikuwa katika mahusiano na rais wa kampuni hiyo Jeff Zucker.

Zucker alijiunga na shirika la CNN mwaka wa 2013 na kabla ya hapo alikuwa ni afisa mkuu mtendaji katika kampuni ya NBC Universal.

View Comments